Vigezo vya kusoma Nursing (Sifa Za Kujiunga)

Vigezo vya kusoma Nursing, Uuguzi ni taaluma muhimu sana katika sekta ya afya. Wauguzi hutoa huduma muhimu kwa wagonjwa na familia zao. Ikiwa unataka kuwa muuguzi, kuna mambo kadhaa muhimu unayohitaji kuzingatia.

Sifa za Kujiunga na Kozi ya Uuguzi

Kabla ya kujiunga na kozi ya uuguzi, kuna sifa kadhaa ambazo ni muhimu kuzingatia:

Lazima uwe na Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) kilichotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

Ufaulu wa alama D katika masomo manne yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi. Kama una ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.

Vigezo vya kujiunga na Uuguzi ngazi ya Cheti

Hapo awali vigezo vya kujiunga na uuguzi ngazi ya cheti vilikuwa vinafanana na kozi nyingine za afya kama maabara, Utabibu, Ufamasia, na Miozi.

 Vigezo ilikuwa ni ufaulu wa alama D katika masomo ya Physics, Chemistry na Biology kwa kidato cha nne. Sasa hivi kujiunga na cheti cha uuguzi lazima uwe na DCC kwenye Physics, Chemistry na Biology.

Muhimu kuzingatia

Hakikisha umepitia Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa Mwaka wa Masomo 2024/2025 na kufahamu mahitaji muhimu na vigezo vya kozi ambayo unataka kuomba katika chuo husika.

Uwe na taarifa zako kamili za kielimu na nyaraka muhimu kama vile cheti cha kuzaliwa, cheti cha kidato cha 4, cheti cha kidato cha 6 kama umehitimu kidato cha 6.

Zingatia ufaulu wako wa kidato cha nne au kidato cha sita uwe umekidhi vigezo kulingana na uhitaji wa kozi ambayo unataka kuomba kama ilivyoonyeshwa kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa Mwaka wa Masomo 2025/2026.

Kusoma Nursing

Shahada Sifa za Uingizaji
Shahada ya Uuguzi Kupata angalau alama C katika kemia na biolojia na angalau alama D katika fizikia.
Stashahada ya Uuguzi au Stashahada ya Juu ya Elimu ya Uuguzi wastani wa “B” au GPA ya chini ya 3.0. Zaidi ya hayo, mwombaji lazima awe na kiwango cha chini cha alama “D” katika masomo yafuatayo: Hisabati, Kemia, Biolojia, Fizikia na Kiingereza katika O-Level.
Cheti cha Uuguzi Lazima uwe na Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) kilichotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA). Ufaulu wa alama D katika masomo manne yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi. Kama una ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.

Mapendekezo:

  1. Vigezo vya kusoma degree ya Pharmacy
  2. Vyuo vinavyotoa kozi ya pharmacy Tanzania
  3. Vyuo vya afya vya serikali Tanzania (Government Health colleges)