Taasisi za mikopo Dar es salaam, Wajasiriamali wadogo na wa kati wanahitaji taarifa mbalimbali zinazohusu huduma za kifedha ili kuendeleza au kuanzisha miradi yao ya kiuchumi na kiufundi.
Shirika la SIDO hutoa mkopo kwa wajasiriamali hadi kiasi cha shilingi 2,500,000 na shilingi 6,000,000 kwa Mfuko ya NEDF na RRF kadhalika. Wajasiriamali ambao wanahitaji kiasi cha fedha zaidi au huduma ya taarifa mbalimbali juu ya mikopo mbalimbali huweza kuunganishwa na SIDO kwenye Taasisi nyingine za kifedha.
Orodha ya baadhi ya Taasisi za kifedha:
- National Microfinance Bank (NMB)
- CRDB Bank PLC
- DCB Bank
- Akiba Commercial Bank
- Equity Bank
Ili kupata maelezo zaidi kuhusu huduma za uunganishwaji wa wajasiriamali kwenye taasisi nyingine za kifedha, mjasiriamali anaweza kuwasiliana na ofisi za SIDO.
Mahitaji ya Kuwasilisha Kufanya Tathmini wa Mkopo:
Benki | Makampuni ya Fedha Ndogo (Microfinance Companies) | SACCOS | |
---|---|---|---|
Leseni hai ya Biashara ya Manispaa/Halmashauri | Leseni hai ya Biashara ya Manispaa/Halmashauri | Leseni hai ya Biashara ya Manispaa/Halmashauri | |
Leseni ya Benki kutoka Benki Kuu Ya Tanzania | |||
Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate) | Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate) | Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate) | |
Hati ya Usajili Kampuni kutoka BRELA | Hati ya Usajili Kampuni kutoka BRELA | Hati ya Usajili Kampuni kutoka BRELA | |
Hati/Memoranda na Makala ya Makubaliano | Hati/Memoranda na Makala ya Makubaliano – Memorandum and Articles of Association (MEMART) | Hati/Memoranda na Makala ya Makubaliano – Memorandum and Articles of Association (MEMART) | |
Mrejesho wa kila mwaka wa BRELA | Mrejesho wa Kila Mwaka wa BRELA | ||
Nakala za Cheti cha Usajili VAT na Utambulisho wa Mlipa Kodi | Nakala za Cheti cha Usajili VAT na Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) | ||
Azimio la Bodi Kukopa | Azimio la Bodi Kukopa | Azimio la Bodi Kukopa | |
Sera ya Mikopo | Sera ya Mikopo | Sera ya Mikopo | |
Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha isiopungua mwaka mmoja nyuma | Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha isiopungua mwaka mmoja nyuma | Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha isiopungua mwaka mmoja nyuma | |
Makadirio ya Mzunguko wa Fedha wa mwaka/miaka ijayo | Makadirio ya Mzunguko wa Fedha wa mwaka/miaka ijayo | Makadirio ya Mzunguko wa Fedha wa mwaka/miaka ijayo | |
Mpango wa Biashara (Business plan) | Mpango wa Biashara (Business plan) | Mpango wa Biashara (Business Plan) |
Benki Kuu ya Tanzania inasimamia taasisi mbalimbali za fedha na inaoorodha ya taasisi hizo. Unaweza kuangalia orodha yao kwa habari zaidi ; https://www.bot.go.tz/BankSupervision/Institutions?lang=sw
Mapendekezo:
Tuachie Maoni Yako