Kata za wilaya ya Mbinga

Kata za wilaya ya Mbinga, Wilaya ya Mbinga ni moja kati ya wilaya nane za Mkoa wa Ruvuma. Makao makuu ya wilaya hiyo yanapatikana Kiamili, kata ya Kigonsera, takribani kilomita 32 kutoka Mbinga Mjini na kilomita 67 kutoka Songea Mjini, ambayo ni makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma.

Eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga lina ukubwa wa kilometa za mraba 6,319.31. Kuna tarafa 5, vijiji 117, na kata 29.

Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imepakana na Wilaya ya Nyasa upande wa kusini na magharibi, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mjini, na Wilaya ya Songea upande wa mashariki, na Wilaya ya Ludewa (Mkoa wa Njombe) upande wa kaskazini.

Orodha ya Kata

Hii ni orodha ya kata za Wilaya ya Mbinga:

Amani Makoro Kambarage Kigonsera
Kihangi Mahuka Kipapa Kipololo
Kitumbalomo Kitura Langiro
Linda Litembo Litumbandyosi
Lukarasi Maguu Mapera
Matiri Mbuji Mhongozi
Mikalanga Mkako Mkumbi
Mpapa Muungano Namswea
Ngima Nyoni Ruanda
Ukata Wukiro

Mapendekezo: