Halmashauri za mkoa wa Ruvuma

Halmashauri za mkoa wa Ruvuma, Mkoa wa Ruvuma ni moja kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Mkoa huu umepewa jina kutokana na Mto Ruvuma, ambao ni mpaka wake wa kusini na nchi ya Msumbiji.

Mkoa wa Ruvuma umepakana na Ziwa Nyasa na Mkoa wa Morogoro upande wa magharibi, mikoa ya Iringa na Lindi upande wa kaskazini, na Mkoa wa Mtwara upande wa mashariki. Makao makuu ya mkoa wa Ruvuma yako Songea mjini.

Mkuu wa Mkoa ni Christine G. Ishengoma. Eneo la mkoa ni kilomita za mraba 63,498. Jumla ya wakazi wote katika mkoa wa Ruvuma ni 1,848,794 (sensa ya mwaka 2022).

Wilaya

Mkoa wa Ruvuma umegawanyika katika wilaya nane:

  1. Namtumbo
  2. Nyasa
  3. Songea Mjini
  4. Songea Vijijini
  5. Tunduru
  6. Madaba
  7. Mbinga Mjini
  8. Mbinga Vijijini

Orodha ya Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma

Hii ni orodha ya halmashauri za Mkoa wa Ruvuma na namba zao za sanduku la posta:

NA JINA LA HALMASHAURI SANDUKU LA POSTA
1 RAS – RUVUMA BOX – 74
2 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA BOX – 14
3 HALMASHAURI YA MJI MBINGA BOX – 134
4 MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA SONGEA BOX – 995
5 MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA NAMTUMBO BOX – 55
6 MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA MADABA BOX – 14
7 MKURURGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA TUNDURU BOX – 275
8 MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMSHAURI YA WILAYA MBINGA BOX – 194

Mapendekezo:

Makabila ya mkoa wa Ruvuma