Faida za kusoma Pharmacy

Faida za kusoma Pharmacy, Famasia ni taaluma muhimu sana katika mfumo wa huduma ya afya. Wafamasia wana jukumu la kuhakikisha kuwa dawa zinatumika kwa usalama na kwa ufanisi. Pia, hutoa ushauri kuhusu matumizi ya dawa na jinsi ya kujiweka na afya njema.

Kwa Nini Usome Famasia?

Kuna faida nyingi za kusoma famasia. Hizi ni pamoja na:

  • Kusaidia watu Ukiwa mfamasia, utaweza kusaidia watu kwa kuwapatia dawa wanazohitaji ili kuboresha afya zao.
  • Kutumia ujuzi wako Famasia inakupa fursa ya kutumia ujuzi wako wa kemia na biolojia kusaidia watu.
  • Fursa za kazi Kuna fursa nyingi za kazi kwa wafamasia, katika hospitali, maduka ya dawa, na makampuni ya dawa.

Kazi za kufanya ukiwa na digrii ya famasia:

  1. Mfamasia
  2. Msimamizi wa huduma ya afya
  3. Mtafiti
  4. Profesa katika chuo kikuu

Sifa za Kujiunga na Kozi ya Famasia

Ili kusoma famasia nchini Tanzania, lazima uwe na sifa zifuatazo:

  • Ufaulu mzuri katika mtihani wa kidato cha nne (CSEE).
  • Ufaulu mzuri katika masomo ya sayansi (Biolojia, Kemia, Fizikia).
  • Shahada ya kwanza ya Famasia kutoka chuo kikuu kinachotambulika.

Hapo chini, kuna jedwali linaloonyesha sifa za kujiunga na kozi ya famasia katika ngazi mbalimbali:

Ngazi ya Elimu Sifa za Kujiunga
Cheti Cheti cha elimu ya sekondari na ufaulu wa daraja la D katika masomo ya Kemia, Baiolojia, Fizikia na somo lingine lolote.
Diploma Cheti cha Ufundi (NTA Level 5) katika Sayansi ya Dawa.
Shahada ya kwanza Mwombaji lazima awe amemaliza elimu ya sekondari ya ngazi ya juu nchini Tanzania na awe na angalau ufaulu watatu wa masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia na awe na alama za chini zaidi za kuingia pointi 6, au sawa na hivyo. Mwombaji lazima awe na angalau D katika Fizikia, Kemia, na Baiolojia.

Vyuo Vikuu vinavyotoa Kozi ya Famasia

Baadhi ya vyuo vikuu vinavyotoa kozi ya famasia nchini Tanzania ni pamoja na:

  • Chuo Kikuu cha katoliki cha Afya na Sayansi Shirikishi (CUHAS)
  • Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Tanzania (KIUT)
  • Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
  • Chuo Kikuu cha St John’s Tanzania (SJUT), Dodoma

Kusoma famasia ni uamuzi mzuri kwa mtu yeyote ambaye anataka kusaidia watu na ana shauku ya sayansi. Kuna fursa nyingi za kazi kwa wafamasia, na taaluma hii inatoa thawabu nyingi.

Mapendekezo:

  1. Vigezo vya kusoma degree ya Pharmacy
  2. Vyuo vinavyotoa kozi ya pharmacy Tanzania
  3. Vyuo vya pharmacy Dar es salaam
  4. Vigezo vya kusoma Nursing (Sifa Za Kujiunga)