Ramani ya mkoa wa Ruvuma na Wilaya zake, Mkoa wa Ruvuma ni moja kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Umepewa jina kutokana na Mto Ruvuma, ambao ni mpaka wake wa kusini na Msumbiji.
Mkoa huu umepakana na Ziwa Nyasa na Mkoa wa Morogoro upande wa magharibi, mikoa ya Iringa na Lindi upande wa kaskazini, na Mkoa wa Mtwara upande wa mashariki. Makao makuu ya mkoa yako Songea mjini.
Wilaya za Mkoa wa Ruvuma
Mkoa wa Ruvuma umegawanyika katika wilaya nane:
- Wilaya ya Nyasa
- Wilaya ya Songea Mjini
- Wilaya ya Songea Vijijini
- Wilaya ya Tunduru
- Wilaya ya Madaba
- Wilaya ya Mbinga Vijijini
- Wilaya ya Mbinga Mjini
- Wilaya ya Namtumbo
Takwimu za Mkoa
Kulingana na sensa ya mwaka 2022, Mkoa wa Ruvuma una jumla ya wakazi 1,848,794. Makabila makubwa katika Ruvuma ni Wangoni, Wamatengo, Wayao, Wandendeule, Wamanda, Wanyasa, Wapoto, Wabena, na Wandengereko.
Jedwali la Wilaya na Idadi ya Wakazi (2022)
Wilaya | Idadi ya Wakazi (2022) |
---|---|
Nyasa | 191,193 |
Songea Mjini | 286,285 |
Songea Vijijini | 178,201 |
Tunduru | 412,054 |
Madaba | 65,215 |
Mbinga Vijijini | 285,582 |
Mbinga Mjini | 158,896 |
Namtumbo | 271,368 |
Historia Fupi ya Wilaya ya Namtumbo
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ilianzishwa rasmi tarehe 02/08/2002. Wilaya hii inakadiriwa kuwa na watu 21 kwa kila kilometa moja ya mraba. Ipo katikati ya Latitudo 9’17’ na Latitudo 11’45’ kusini mwa mstari wa Ikweta na pia katikati ya Longitudo 35’57’ na Longitudo 36’52’ kutoka mashariki mwa GMT.
Wilaya ya Namtumbo imepakana na Songea upande wa Magharibi, Wilaya ya Ulanga (Mkoa wa Morogoro) kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Tunduru na Liwale (Mkoa wa Lindi) upande wa Mashariki. Upande wa kusini kuna Mto Ruvuma na mpaka wa kimataifa wa Nchi ya Msumbiji.
Mawasiliano ya Halmashauri za Mkoa
Kwa mawasiliano na halmashauri za mkoa wa Ruvuma, unaweza kutumia anwani zifuatazo:
- RAS – Ruvuma, Sanduku la Posta 74
- Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Sanduku la Posta 14
- Halmashauri ya Mji Mbinga, Sanduku la Posta 134
- Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Songea, Sanduku la Posta 995
- Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Namtumbo, Sanduku la Posta 55
- Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Madaba, Sanduku la Posta 14
- Mkururgenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Tunduru, Sanduku la Posta 275
- Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga, Sanduku la Posta 194
Mapendekezo:
Tuachie Maoni Yako