Mkoa wa ruvuma una wilaya ngapi? wikipedia, Mkoa wa Ruvuma ni moja kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Imepewa jina kutokana na mto Ruvuma ambao ni mpaka wake wa kusini na Msumbiji.
Mkoa wa Ruvuma umepakana na Ziwa Nyasa na Mkoa wa Morogoro upande wa magharibi, mikoa ya Iringa na Lindi upande wa kaskazini na Mkoa wa Mtwara upande wa mashariki. Makao makuu ya mkoa yako Songea mjini.
Jiografia
Mkoa wa Ruvuma unapatikana katika nyanda za juu kusini, ambazo huanzia mita 300 hadi 2000 juu ya usawa wa bahari. Sehemu ya magharibi ya Mkoa imefunikwa na Ziwa Nyasa ambalo liko ndani ya ufa wa magharibi.
Upande wa mashariki wa Bonde la Ufa kuna safu za Milima ya Matengo ambayo hupanda hadi mita 2000. Vile vile kuelekea Kaskazini kuna Milima ya Lukumburu ambayo mwinuko wake uko hadi mita 2000 juu ya usawa wa bahari. Kusini mwa Mkoa hupitia tambarare za chini ambazo zimekatwa na mto Ruvuma.
Wilaya
Mkoa wa Ruvuma una wilaya nane:
- Wilaya ya Nyasa
- Wilaya ya Songea Mjini
- Wilaya ya Songea Vijijini
- Wilaya ya Tunduru
- Wilaya ya Madaba
- Wilaya ya Mbinga Vijijini
- Wilaya ya Mbinga Mjini
- Wilaya ya Namtumbo
Wilaya |
---|
Nyasa |
Songea Mjini |
Songea Vijijini |
Tunduru |
Madaba |
Mbinga Vijijini |
Mbinga Mjini |
Namtumbo |
Wakazi
Jumla ya wakazi wote katika Mkoa wa Ruvuma ni 1,848,794 (sensa ya mwaka 2022). Makabila makubwa katika Ruvuma ni Wangoni, Wamatengo, Wayao, Wandendeule, Wamanda, Wanyasa, Wapoto, Wabena na Wandengereko.
Makala Nyingine:
Tuachie Maoni Yako