Nafasi za Kazi Jeshi la Zimamoto 2025 ajira zimamoto 2025 Jinsi Ya Kutuma Maombi ajira.zimamoto.go.tz Ajira za,Tangazo la ajira zimamoto 2025/2026 pdf Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetangaza nafasi mpya za ajira kwa vijana wa Kitanzania waliohitimu kidato cha nne na ngazi ya shahada. Nafasi hizo zitatolewa kwa ngazi ya Konstebo kwa wale wanaokidhi vigezo vilivyoainishwa.
Taarifa hii imetolewa rasmi leo, Alhamisi, Februari 13, 2025, na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, John Masunga. Ingawa idadi ya nafasi za kazi haijawekwa wazi, waombaji wanahimizwa kutuma maombi kabla ya tarehe ya mwisho, Februari 28, Mwaka 2025.
Vigezo vya Kustahiki Ajira
Waombaji wanapaswa kukidhi masharti yafuatayo:
Sifa | Maelezo |
---|---|
Uraia | Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa |
Umri | Miaka 18 – 25 kwa waombaji wa kawaida, 18 – 35 kwa marubani wa helikopta |
Urefu | Wanaume: Futi 5.7+, Wanawake: Futi 5.4+ |
Afya | Awe na afya njema kimwili na kiakili |
Tabia | Asiwe na rekodi ya uhalifu, asiwe na tattoo mwilini |
Ndoa | Asiwe ameoa au kuolewa |
Ajira ya awali | Asiwe ameajiriwa serikalini hapo awali |
Sifa za Ziada kwa Wenye Ujuzi Maalum
Jeshi limeeleza kuwa waombaji wenye taaluma au ujuzi ufuatao wanapewa kipaumbele:
- Udereva wa magari makubwa (leseni daraja E, umri miaka 18-28)
- Ufundi bomba
- Uuguzi
- Taaluma ya Zimamoto na Uokoaji
- Utabibu
- Urubani wa helikopta
Kwa waombaji wenye shahada, fani zinazopendelewa ni:
- Uhandisi wa bahari na ndege
- Lugha (Kiingereza)
- Ukadiriaji majenzi
- Teknolojia ya habari
- Uchumi
- Sheria (waliomaliza shule ya sheria kwa vitendo)
- Ualimu
- Usafirishaji barabara na reli
- Uhandisi wa kemikali
Jinsi ya Kuomba
Waombaji wanapaswa kutuma maombi kupitia mfumo rasmi wa ajira wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unaopatikana kupitia kiunganishi:
👉 ajira.zimamoto.go.tz
Nyaraka Muhimu za Kuambatisha
- Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa
- Fomu ya uthibitisho wa afya kutoka kwa mganga wa serikali
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya NIDA
- Picha ya pasipoti ya hivi karibuni
- Namba ya mtihani wa kidato cha nne
Waombaji wote wanahimizwa kuzingatia vigezo vyote na kutuma maombi kabla ya tarehe 28 Februari 2025.
🔴 Tangazo hili halihusishi malipo yoyote katika mchakato wa kuomba ajira.
Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti rasmi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji au ofisi zao zilizo karibu nawe.
Soma Makala Nyingine:
Fomu ya Uchunguzi wa Afya (PDF)
Kwa wale ambao wamesomea course ya maendeleo ya jamii wanaweza kupata kipaumbele
I face challenge in password when I try to forgot it brought link at mid night when I wake it has expired sorry I need you are help In my password
It Look like your web developer stuck in a washing machines
Serikali imetuacha mtaani muda mrefu mpaka leo tunashindwa kuomba nafasi mbalimbali za kazi eti kwa kigezo cha umri, yaani kwakuwa nina umri wa miaka 30 basi siwezi kuajiriwa eti kutokana na umri ni mkubwa
Sasa katika hili nani alaumiwe, sio kosa langu ila hii wameweka vigezo ambavyo sio sawa tumemaliza vyuo muda mrefu ajira zinatolewa chache tena zinabana wengine, yani hii ndiyo ile mtoto ulimuacha shule bado mdogo wewe umemaliza hadi chuo muda then yeye anakuja kupata ajira kabla yako eti kwa kuwa ana umri sahihi yaani miaka 18 – 28 hili jambo linaongeza sana chuki dhidi ya serikali kwani wanatuambia vigezo ambavyo vinakandamiza wasomi wa muda mrefu ambao wao wenyewe ndiyo wamewakosesha ajira
INAUMA SANA HILI ILA IPO SIKU TUTAPATA MTETEZI
UBAGUZI WA KI UMRI UMEJITOKEZA