Nafasi za kazi UTUMISHI Zanzibar 2025 Ajira Mpya, Kupitia Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (OR-KSUUB), Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (OR-KSUUB) imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi, kuimarisha utawala bora na kuwezesha utendaji kazi wenye ufanisi katika utumishi wa umma.
OR-KSUUB ina jukumu la kusimamia masuala yote yahusuyo utumishi wa umma, sheria, haki za binadamu, utawala bora, serikali mtandao na usimamizi wa nyaraka. Hii ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2050 na Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025.
DIRA YA OFISI
Kuwa na jamii inayoheshimu misingi ya utumishi, haki, usawa, sheria na utawala bora.
DHAMIRA
Kuimarisha maendeleo ya utumishi wa umma na kuweka misingi ya usawa, sheria na upatikanaji wa haki kwa kuzingatia utawala bora.
LENGO
Kuimarisha utendaji kazi katika utumishi wa umma na kuratibu masuala ya Katiba, Sheria, Utawala Bora pamoja na mahusiano ya kikanda na kimataifa.
NAFASI ZA AJIRA 2025
Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora inatarajia kutangaza nafasi mbalimbali za kazi kwa mwaka 2025. Fursa hizi ni kwa watanzania wenye sifa stahiki kuomba ajira katika kada mbalimbali zitakazotangazwa kupitia tovuti rasmi ya ofisi hiyo.
Baadhi ya Kada Zinazotarajiwa Kutangazwa:
- Maafisa Utumishi
- Maafisa Sheria
- Wakaguzi wa Ndani
- Wahifadhi Kumbukumbu
- Wataalamu wa TEHAMA
- Wasaidizi wa Kumbukumbu
- Wasaidizi wa Sheria
https://utumishismz.go.tz/tangazo_zaid/
SIFA ZA WAOMBAJI
- Awe raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.
- Awe na elimu na taaluma inayolingana na nafasi husika.
- Awe hana rekodi ya makosa ya jinai au mwenendo mbaya kazini.
- Awe tayari kufanya kazi katika mazingira yoyote ya Zanzibar.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Waombaji wote wanapaswa kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia tovuti rasmi ya OR-KSUUB:
Hatua za Kuomba:
- Tembelea tovuti hiyo na bonyeza sehemu ya Ajira Mpya.
- Jisajili kwa kujaza taarifa zako binafsi na za kitaaluma.
- Chagua nafasi unayoomba na pakia vyeti vyako.
- Hakikisha unathibitisha maombi yako kabla ya kuwasilisha.
NB: Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au mikono hayatapokelewa.
MAWASILIANO RASMI
Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (OR-KSUUB)
Barabara ya Julius Nyerere, Mazizini
P.O Box 3356, Zanzibar
Simu: +255 024 2230038 / +255 024 2452294
Simu ya mkononi: +255 77000000
Fax: +255 024 2230027 / +255 024 2452291
Barua Pepe: [email protected]
Kwa Habari Zaidi na Tangazo Rasmi la Ajira:
Fuatilia tovuti: https://utumishismz.go.tz
Makala Nyingine: