Nafasi Za Kazi Shirika La Utangazaji Tanzania (TBC) 22-10-2024

Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)”TANZANIA BROADCASTING CORPORATION”, inawatangazia Watanzania wenye sifa, ujuzi na uzoefu kutuma maombi ya kujaza nafasi 25 za kazi zilizoainishwa hapa chini.

1. Mhandisi Daraja la II (Mawasiliano ya Kielektroniki) – Nafasi 8

Majukumu:

  • Kufanya kazi za kiteknolojia, usakinishaji, huduma na matengenezo ya vifaa vya redio na televisheni.
  • Kutayarisha makadirio ya gharama za miradi ya kielektroniki.
  • Kuandaa ripoti za kiufundi.
  • Kukagua maeneo ya kazi na kuandaa ripoti za ukaguzi.

Sifa:

  • Shahada ya Uhandisi wa Mawasiliano au Uhandisi wa Kielektroniki na Umeme kutoka chuo kinachotambulika.
  • Lazima uwe umejisajili na bodi husika kama Mhandisi Mhitimu.

Mshahara: TBCSS – 5.

2. Afisa TEHAMA Daraja la II (Viwango na Uzingatiaji) – Nafasi 1

Majukumu:

  • Kuweka mipango ya viwango na miongozo ya TEHAMA.
  • Kufanya tathmini ya mwenendo wa viwango vya TEHAMA duniani.
  • Kuratibu uandaaji wa vipimo vya vifaa vya teknolojia ya habari.

Sifa:

  • Shahada ya Sayansi ya Kompyuta au Teknolojia ya Habari kutoka chuo kinachotambulika.
  • Cheti cha CISA, CISM, CISSP, CEH, TOGAF na CCNA kitakuwa faida.

Mshahara: TBCSS – 5.

3. Afisa TEHAMA Daraja la II (Msimamizi wa Programu) – Nafasi 1

Majukumu:

  • Kusimamia mifumo ya matumizi ya utangazaji wa redio na televisheni.
  • Kufanya usakinishaji, usasishaji na matengenezo ya mifumo.

Sifa:

  • Shahada ya Sayansi ya Kompyuta au Uhandisi wa Kompyuta.
  • Ujuzi katika AVRA Radio Broadcasting na SI Media Television Broadcasting utakuwa faida.

Mshahara: TBCSS – 5.

4. Afisa TEHAMA Daraja la II (Msimamizi wa Hifadhidata) – Nafasi 1

Majukumu:

  • Kubuni miundo ya hifadhidata na kufanya uboreshaji wa utendaji wa hifadhidata.

Sifa:

  • Shahada ya Sayansi ya Kompyuta au Teknolojia ya Habari.
  • Ujuzi katika Usalama wa Mtandao na mifumo ya Linux na Windows ni faida.

Mshahara: TBCSS – 5.

5. Afisa TEHAMA Daraja la II (Msimamizi wa Mtandao) – Nafasi 1

Majukumu:

  • Kufanya usanifu na upanuzi wa uwezo wa mtandao.
  • Kusimamia mifumo ya usalama kama vile firewall na antivirus.

Sifa:

  • Shahada ya Sayansi ya Kompyuta au Uhandisi wa Kompyuta.

Mshahara: TBCSS – 5.

6. Mwandishi wa Habari Daraja la II – Nafasi 5

Majukumu:

  • Kukusanya na kuandika habari.
  • Kuandaa na kuhariri matangazo ya redio na televisheni.

Sifa:

  • Shahada au Diploma ya Juu ya Uandishi wa Habari au Mawasiliano ya Umma.
  • Ujuzi wa kutumia programu za kompyuta na uhariri wa picha ni faida.

Mshahara: TBCSS – 4.

7. Mhariri Daraja la II – Nafasi 8

Majukumu:

  • Kusaidia kuhariri vipindi vya televisheni.
  • Kuandaa filamu na kuzihariri ili kufikia malengo ya mzalishaji.

Sifa:

  • Shahada au Diploma ya Juu katika Sanaa za Maonyesho, Uandishi wa Habari, au Mawasiliano ya Umma.

Mshahara: TBCSS – 4.

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  • Waombaji lazima wawe raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45.
  • Watu wenye ulemavu wanahimizwa kuomba.
  • Maombi yatumwe kupitia tovuti: http://portal.ajira.go.tz/
  • Mwisho wa kutuma maombi: 4 Novemba, 2024.

Chanzo: Taarifa ya nafasi za kazi kutoka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma​

PDF Hapa; 20242210441621TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI TBC

Nafasi Za Kazi Nyingine: