Tangazo La Nafasi Za Kazi Ofisi Ya Waziri Mkuu-sera,bunge Na Uratibu 23-05-2025, Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi nane (08) kama ifuatavyo:
1. MPIGA CHAPA MSAIDIZI DARAJA II (ASSISTANT PRINTER II)
Idadi ya Nafasi: 08
Mahali: Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu
1.1 Majukumu ya Kazi
- Kukunja karatasi ngumu na kutengeneza jalada (covers) za vitabu, majarida na madaftari kwa njia ya kugandisha, kushona au kuunganisha.
- Kukarabati vitabu au kumbukumbu kwa kuweka jalada jipya au kurudisha katika hali ya awali.
- Kupanga vifaa vilivyotengenezwa kwa vipimo au seti husika.
- Kuendesha mashine za kupiga chapa, kukata karatasi, kushona au kugandisha vitabu kwa mujibu wa ubora unaotakiwa.
- Kupanga karatasi za kuchapwa kwa hesabu ya kila nakala (kitabu, jarida, daftari, n.k).
1.2 Sifa za Muombaji
- Awe amehitimu kidato cha Nne au Sita katika masomo ya Sayansi au Sanaa.
- Awe na cheti cha Trade Test daraja la I au Level III katika Lithography, Composing, Binding au Machine Binding.
- Au awe amehitimu mafunzo ya miaka miwili ya kupiga chapa.
1.3 Ngazi ya Mshahara
-
Kwa mujibu wa viwango vya Serikali: TGS B
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Awe Raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45 (isipokuwa kwa walioko kazini Serikalini).
- Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja aina ya ulemavu kwenye mfumo wa maombi.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na mwanasheria/wakili.
- Watumishi wa Umma wanaotaka kuhamia kada nyingine lazima wapitishe barua zao kwa waajiri wao wa sasa.
- Maombi yaambatane na:
-
- CV iliyoandikwa kwa kina (anwani, simu, na majina ya wadhamini watatu).
- Nakali halisi zilizothibitishwa za vyeti vya taaluma na kitaaluma:
- Cheti cha kuzaliwa
- Cheti cha kidato cha Nne na Sita (kwa waliofikia)
- Vyeti vya mafunzo ya ufundi/stashahada/astashahada
- Vyeti vya kompyuta
- Vyeti vya kitaaluma (kutoka bodi husika)
- HAKUTAKUBALIWA: “Provisional Results”, “Statement of Results”, na “Slips”.
- Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuthibitishwa na NECTA, NACTE au TCU.
- Waliostaafu Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa idhini ya Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji walioajiriwa katika nafasi sawa za kuingilia katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.
- Watakaotoa taarifa au vyeti vya kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 05 Juni, 2025
MAELEKEZO YA UWASILISHAJI WA MAOMBI:
Maombi yote ya kazi yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia Mfumo wa Ajira wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma https://portal.ajira.go.tz/user/auth/login. Kumbuka kuambatisha barua ya maombi iliyoandikwa kwa ufasaha, imesainiwa na kuelekezwa kwa:
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Makala Nyingine: