Nafasi Za kazi Mtendaji wa Kijiji Daraja la III Kigoma Oktoba, 2024

Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa stahiki kwa ajili ya nafasi ya Mtendaji wa Kijiji Daraja la III. Nafasi hizi zinahusisha majukumu ya kusimamia uendeshaji wa shughuli za kijiji na utekelezaji wa sera za serikali katika ngazi ya kijiji. Maombi yanaweza kuwasilishwa kuanzia tarehe 28 Septemba 2024 hadi 11 Oktoba 2024.

MTENDAJI WA KIJIJI III – 8 POSTS

Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Application Timeline: 2024-09-28 to 2024-10-11

Job Summary

N/A

Majukumu

  • Afisa Masuuli na mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji;
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji;
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji;
  • Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
  • Kutafsiri na kusimamia sera, sheria, na taratibu;
  • Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
  • Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalam katika kijiji;
  • Kusimamia, kukusanya, na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji;
  • Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji;
  • Kupokea, kusikiliza, na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
  • Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji;
  • Kuwajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata.

Vigezo Na Uzoefu

Kuajiriwa mwenye elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii, au Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

Mshahara

TGS B

Jinsi Ya Kutuma Maombi

Tuma Maombi Hapa