NAFASI ZA KAZI JESHI LA POLISI TANZANIA 2025/2026 AJIRA

NAFASI ZA KAZI JESHI LA POLISI TANZANIA 2025/2026 Ajira Mpya Tangazo la kazi kutoka jeshi la polisi.

Nafasi za kazi Jeshi la polisi 2025 Ajira Mpya Polisi 2025/2026, www.polisi.go.tz ajira. Ajira mpya jeshi la polisi 2025 Tangazo La nafasi za kazi polisi lipo kwenye PDF.

NAFASI ZA KAZI JESHI LA POLISI

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania ametangaza nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania kwa mwaka wa 2025/2026. Nafasi hizi zinapatikana kwa wale wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha Sita na Kidato cha Nne.

SIFA ZA MWOMBAJI

Sifa Maelezo
Uraia Awe raia wa Tanzania na wazazi wake wawe raia wa Tanzania.
Elimu Kidato cha Nne au Sita (2019 – 2025), Astashahada, Stashahada, Shahada.
Umri Kidato cha Nne/Sita: Miaka 18 – 25; Shahada/Stashahada: Miaka 18 – 30.
Ufaulu Kidato cha Nne: Division I – IV (Pointi 26 – 28 kwa Division IV); Kidato cha Sita: Division I – III.
Urefu Wanaume: 5’8″, Wanawake: 5’4″.
Lugha Kiswahili na Kingereza kwa ufasaha.
Afya Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa serikali.
NID Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka NIDA.
Ndoa Awe hajaoa/kuolewa na asiwe na watoto.
Uadilifu Asiwe na kumbukumbu za uhalifu, asiwe na tattoo, asiwe mtumiaji wa dawa za kulevya.
Ajira Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya serikali.
Kujitolea Awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote Tanzania.

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI

Waombaji wote waandike barua za maombi kwa mkono (Handwriting) wakitaja namba zao za simu.

Barua hiyo ipelekwe kwa anuani ifuatayo:

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania
S.L.P 961,
DODOMA.

Barua iambatishwe na nakala ya nyaraka husika katika mfumo wa PDF.

Maombi yafanywe kupitia mfumo wa Ajira wa Polisi unaopatikana kwenye tovuti: https://ajira.tpf.go.tz.

Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta, barua pepe au kwa mkono hayatapokelewa.

MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI

04 Aprili 2025

PDF YA KADA ZOTE ZILIZOTANGAZWA

📄 Pakua hapa: TANGAZO_LA_NAFASI_ZA_AJIRA_ZA_POLISI

IMETOLEWA NA:

📌 Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania
📍 Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,
📬 S.L.P 961, DODOMA.
🗓️ Tarehe: 20/03/2025

🔗 Tembelea: www.polisi.go.tz kwa maelezo zaidi:

Mapendekezo:

  1. Nafasi za kazi Jeshi la polisi 2025 Ajira Mpya (Tangazo)
  2. Mfumo wa ajira polisi www polisi.go.tz ajira 2025
  3. Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi Jeshi la Polisi (Sample)
  4. Majukumu ya Jeshi la Polisi Tanzania
  5. Vyeo vya Polisi Tanzania
  6. Sifa Za Mwombaji Ajira Jeshi la Polisi 2025 (Vigezo Vya Kujiunga)
  7. Plate number za Magari ya serikali