Nafasi za kazi Jeshi la Magereza Agosti, 2025 ajira mpya (Ajira magereza pdf) Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, anawatangazia vijana wote wa Kitanzania wenye sifa stahiki nafasi za ajira kwa wahitimu wa Kidato cha Nne (Form IV) na wenye ujuzi katika fani mbalimbali kwa ngazi ya Stashahada na Shahada kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe Raia wa Tanzania.
- Awe na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Uraia (NIDA).
- Asiwe amewahi kuajiriwa Serikalini.
- Awe na umri kati ya miaka 18 – 24 kwa wahitimu wa Kidato cha Nne, na 18 – 28 kwa wenye ujuzi.
- Awe na Cheti cha Kuzaliwa.
- Awe na urefu usiopungua futi 5’4″ kwa wanawake na futi 5’7″ kwa wanaume.
- Awe na afya njema ya mwili na akili iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali.
- Asiwe ameoa/kuolewa na asiwe amewahi kujifungua.
- Asiwe na alama au michoro (tattoo) mwilini.
- Awe na nidhamu na tabia njema, asiwe na rekodi ya kosa la jinai.
- Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya askari magereza na kufanya kazi sehemu yoyote Tanzania Bara.
- Awe tayari kujigharamia hatua zote za awali za usaili hadi kuripoti mafunzoni.
UJUZI NA FANI ZINAZOHITAJIKA
- Shahada:
-
- Uhandisi wa Programu (Software Engineering)
- Sayansi ya Teknolojia ya Vyombo vya Habari Mseto na Uhuishaji (Multimedia & Animation)
- Usalama wa Mifumo (Cyber Security)
- Uhandisi wa Mitandao (Network Engineering)
- Saikolojia na Ushauri Nasaha (Psychology & Counselling)
- Uhandisi wa Uchimbaji Madini (Mining Engineering)
- Stashahada:
- Ufundi wa Vifaa vya Ofisi (Office Machine)
- Lugha za Alama (Sign Language)
- Kilimo (Agriculture)
- Uuguzi (Nursing)
- Mitambo ya Kilimo (Agro-mechanization)
- Mifugo (Animal Health and Production)
- Astashahada:
- Katibu Muhtasi (Secretarial Studies)
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yatume kupitia Mfumo wa Ajira wa Jeshi la Magereza (TPSRMS) kwa anuani:
👉 https://ajira.magereza.go.tz
Maombi yatakayowasilishwa kwa njia nyingine hayatapokelewa.
MATANGAZO
Tangazo kamili la Ajira Jeshi la Magereza Tanzania 2025 linapatikana hapa:
📄 Pakua Tangazo (PDF)
Mwisho wa kutuma maombi: 29 Agosti, 2025
ZINGATIA
- Waombaji wote waliowahi kufukuzwa mafunzo ya awali ya askari magereza hawaruhusiwi kuomba tena.
- Mtu yeyote atakayewasilisha nyaraka za kughushi au kuficha sifa za kweli atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Makala Nyingine;
- Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Magereza (Mfano)
- Jinsi ya kuomba ajira magereza (Kutuma Maombi)
- Muundo wa jeshi la magereza
- Historia ya jeshi la magereza
- Mshahara wa jeshi la magereza
- Mafunzo ya askari magereza
Ajira za Magereza 2025 Magereza – ajira.magereza.go.tz
Taarifa Zaidi:
Jeshi la Magereza Tanzania ajira.magereza.go.tz
maombi ya ajira jeshi la magereza
Janeth charles
Naomba nisaidiwe jinsi ya kutuma maombi
Fom lv