Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu anawatangazia Watanzania wote wenye sifa kutuma maombi ya ajira kwa nafasi zilizoidhinishwa kupitia kibali cha ajira mpya kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kama ifuatavyo:
1. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 5
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI).
- Leseni ya Daraja “C” au “E”.
- Uzoefu wa kuendesha magari kwa mwaka 1 bila kusababisha ajali.
- Cheti cha mafunzo ya uendeshaji kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Majukumu:
- Kukagua gari kabla/baada ya safari.
- Kuwasafirisha watumishi.
- Matengenezo madogo ya gari.
- Kusambaza nyaraka na kutunza logbook.
- Kufanya usafi wa gari na kazi nyingine kwa maelekezo ya msimamizi.
Mshahara:
- Ngazi ya Mshahara: TGS B
2. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 6
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
- Stashahada ya Uhazili (NTA Level 6).
- Uwezo wa Hatimkato Kiswahili na Kiingereza (maneno 100 kwa dakika).
- Ujuzi wa programu za kompyuta: Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher.
Majukumu:
- Kuchapa nyaraka na barua za kawaida na siri.
- Kupokea wageni na kuwasiliana kuhusu mahitaji yao.
- Kutunza ratiba, kumbukumbu na majalada.
- Kusaidia maandalizi ya vikao na vifaa vya ofisi.
Mshahara:
- Ngazi ya Mshahara: TGS C
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI:
- Mwombaji awe Mtanzania mwenye umri kati ya miaka 18 – 45 (isipokuwa waajiriwa wa Serikali).
- Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kuainisha aina ya ulemavu wao kwenye mfumo wa maombi.
- Aambatishe CV, anuani, namba za simu, barua pepe, na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika.
- Vyeti vya elimu na taaluma vihalalishwe na Mwanasheria/Wakili.
- “Statement of results”, “Provisional Results”, “Results Slips” hazikubaliki.
- Waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU, NECTA au NACTE.
- Wastaafu wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waajiriwa katika nafasi za kuingilia hawapaswi kuomba.
- Maombi ya sifa au taarifa za kughushi yatapelekea hatua za kisheria.
MAELEKEZO YA UOMBANJI:
Maombi yaambatane na barua ya maombi iliyosainiwa na vyeti vyote vya elimu.
Barua ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
S.L.P. 50,
USHETU – KAHAMA
Maombi yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira: https://portal.ajira.go.tz
Mwisho wa kutuma maombi: 09 Juni 2025
Imetolewa na:
Hadija M. Kabojela
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu