Ajira

Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Tanganyika Mei, 2025

Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Tanganyika Mei, 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika anatangaza nafasi za kazi kwa wananchi wote wa Tanzania waliokidhi vigezo.

Kibali cha ajira kimetolewa na Katibu Mkuu – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua ya tarehe 29 Aprili, 2025.

1.0 NAFASI ZINAZOTANGAZWA

1.1 Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II (Nafasi 5)

Majukumu ni pamoja na kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka, kusambaza na kurudisha majalada, kutafuta kumbukumbu zinazohitajika na kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi.

Sifa ni kuhitimu kidato cha nne au sita, na kuwa na Stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali. Mwombaji awe na ujuzi wa kompyuta.
Ngazi ya mshahara: TGS C.

1.2 Dereva Daraja la II (Nafasi 6)

Majukumu ni pamoja na kukagua gari kabla na baada ya safari, kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi, kufanya matengenezo madogo ya gari, kufanya usafi wa gari na kusambaza nyaraka.

Sifa ni kuwa na cheti cha kidato cha nne, leseni ya daraja E au C, uzoefu wa mwaka mmoja bila kusababisha ajali, na cheti cha mafunzo ya msingi ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Ngazi ya mshahara: TGS B.

2.0 MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  1. Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
  2. Aambatishe nakala za vyeti vya elimu ya sekondari, taaluma, nakala ya kadi ya NIDA au namba ya NIDA, na cheti cha kuzaliwa.
  3. Result Slip, Statement of Results, Provisional Results au Transcripts hazitakubaliwa.
  4. Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na waeleze aina ya ulemavu walionao.
  5. Waambatishe CV iliyo na maelezo ya kutosha, anuani, namba ya simu, barua pepe, na majina ya wadhamini watatu.
  6. Waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU, NECTA au NACTE.
  7. Wastaafu hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali kutoka Katibu Mkuu Kiongozi.
  8. Waombaji waote watakaowasilisha taarifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
  9. Watakaokidhi vigezo tu ndio wataitwa kwenye usaili.
  10. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 02 Juni, 2025.

3.0 NAMNA YA KUTUMA MAOMBI

Barua ya maombi ya kazi iwe imeandikwa kwa ufasaha na kusainiwa. Iambatane na vyeti vyote muhimu vya elimu na taaluma. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,
S.L.P. 1, MPANDA.

Maombi yote yawasilishwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anwani:
👉 https://portal.ajira.go.tz

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu huu hayatafanyiwa kazi.

Imetolewa na:
Shaban J. Juma
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika

Makala Nyingine:

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.