Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea amepokea kibali cha ajira kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Hivyo, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kwa nafasi zifuatazo:
1. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 05
Majukumu:
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri.
- Kupokea na kuelekeza wageni.
- Kutunza kumbukumbu za matukio, vikao na safari za mkuu wake.
- Kupokea na kusambaza majalada.
- Kuandaa vifaa vya ofisi na maandalizi ya vikao.
- Kutekeleza kazi nyingine utakazopangiwa na mkuu wa kazi.
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV).
- Diploma ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili.
- Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza (maneno 80 kwa dakika).
- Ujuzi wa programu za ofisi (Word, Excel, PowerPoint, Email, Internet, Publisher).
Ngazi ya Mshahara: TGS C1
2. Dereva Daraja la II – Nafasi 03
Majukumu:
- Kukagua gari kabla/baada ya safari.
- Kuwapeleka watumishi safarini.
- Kufanya matengenezo madogo ya gari.
- Kusambaza nyaraka.
- Kuweka kumbukumbu za safari na kufanya usafi wa gari.
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha Nne au Sita.
- Leseni ya Daraja C au E yenye uzoefu wa mwaka 1 bila ajali.
- Mafunzo ya msingi ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Ngazi ya Mshahara: TGS B1
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Raia wa Tanzania, umri miaka 18 hadi 45.
- Ambatanisha CV yenye anwani, simu, barua pepe na referees 3 wa kuaminika.
- Watumishi wa umma waambatanishe barua kupitia kwa waajiri wao.
- Vyeti vyote vya elimu na taaluma viwe vimehakikiwa na Mwanasheria/Wakili.
- Hati za matokeo (Statement of Results), Provisional na Testmonials HAZITAKUBALIWA.
- Waliosoma nje wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU/NECTA/NACTE.
- Waliostaafu hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Taarifa/sifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi: 10 Juni, 2025.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI:
Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa Ajira Portal: https://portal.ajira.go.tz
Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu hayatafanyiwa kazi.
Anwani ya barua:
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Barabara ya Halmashauri
S. L. P 995
57183, SONGEA – RUVUMA
Imetolewa na:
Elizabeth M. Gumbo
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA