Ajira

Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Singida Juni, 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida anawatangazia Watanzania wote wenye sifa kuomba nafasi za ajira zilizoidhinishwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 na 2024/2025 kama ifuatavyo:

1. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 5

Sifa za Mwombaji:

  • Awe amefaulu Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI).
  • Awe na Stashahada (Diploma) au NTA Level 6 ya Uhazili.
  • Awe amefaulu somo la Hatimkato kwa Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika.
  • Awe na ujuzi wa programu za kompyuta: Word, Excel, PowerPoint, Email, Internet na Publisher.

Majukumu:

  • Kuchapa barua na nyaraka za kawaida na za siri.
  • Kupokea wageni na kuelekeza huduma.
  • Kutunza kumbukumbu na ratiba za Mkuu wake.
  • Kusaidia maandalizi ya vikao na orodha ya vifaa.

Mshahara:

  • Ngazi ya Serikali: TGS C.

2. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 3

Sifa za Mwombaji:

  • Cheti cha Kidato cha Nne (IV).
  • Leseni ya daraja “C” au “E” na uzoefu wa kuendesha bila ajali angalau mwaka 1.
  • Cheti cha Mafunzo ya Uendeshaji kutoka VETA au chuo kinachotambulika na Serikali.

Majukumu:

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari.
  • Kuwasafirisha watumishi na nyaraka.
  • Kuweka rekodi za safari (logbook) na kufanya usafi wa gari.
  • Kufanya matengenezo madogo na kazi nyingine zitakazoelekezwa.

Mshahara:

  • Ngazi ya Serikali: TGS B.

MASHARTI YA JUMLA:

  • Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45.
  • Aambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
  • Awe na wasifu binafsi (CV) ulio kamili na picha mbili za “passport size”.
  • Aambatishe vyeti halisi vya taaluma vinavyotambulika na Serikali.
  • “Statement of Results” na “Provisional Results” hazikubaliki.

Waliomaliza masomo nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na NECTA, NACTE au TCU.

  • Wastaafu hawaruhusiwi kuomba bila kibali maalum.
  • Waajiriwa wa Serikali waliopo katika nafasi za kuingilia hawapaswi kuomba.

MAELEKEZO YA UOMBANJI:

Barua ya maombi ielekezwe kwa:

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Singida
S.L.P. 27, SINGIDA

Maombi yote yawasilishwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira:
👉 https://portal.ajira.go.tz

Mwisho wa kutuma maombi: 10 Juni 2025

Imetolewa na:

Ester Chaula
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Singida

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.