Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale amepokea kibali cha ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu – Utumishi kwa ajili ya mwaka wa fedha 2024/2025. Hivyo, anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kwa nafasi zifuatazo:
1. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 04
Majukumu:
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri.
- Kupokea na kuelekeza wageni.
- Kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, vikao na safari za mkuu wake.
- Kupokea na kusambaza majalada kwa maofisa husika.
- Kuandaa mahitaji ya vifaa vya ofisi na maandalizi ya vikao.
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya kidato cha Nne au Sita.
- Diploma ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6.
- Uwezo wa hati mkato wa Kiswahili na Kiingereza (maneno 100 kwa dakika).
- Ujuzi wa programu za ofisi kama Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, na Publisher.
Ngazi ya Mshahara: TGS C
2. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 02
Majukumu:
- Kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka kwenye rejista.
- Kusambaza na kurudisha majalada kwa watendaji.
- Kuchambua, kupanga na kuhifadhi nyaraka kulingana na somo husika.
- Kutunza mafaili kwenye masijala.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi.
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya kidato cha Nne au Sita.
- Diploma ya Masijala (NTA Level 6) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Ujuzi wa kutumia kompyuta.
Ngazi ya Mshahara: TGS C
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Awe Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45 (isipokuwa walioko Serikalini).
- Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kuainisha aina ya ulemavu kwenye mfumo.
- Ambatanisha CV, anwani, barua pepe, simu, na majina ya wadhamini 3.
- Ambatanisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Wakili.
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of Results” HAZITAKUBALIWA.
- Waliosoma nje wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU/NECTA/NACTVET.
- Wastaafu wa umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Watumishi wa umma walioko katika nafasi za kuingilia wasitume maombi.
- Sifa au taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 12 Juni, 2025.
MUHIMU:
Barua ya maombi iliyosainiwa ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 352,
NYANG’HWALE
Namna ya Kutuma Maombi:
Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa Ajira Portal: https://portal.ajira.go.tz
Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu hayatafanyiwa kazi.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG’HWALE