Ajira

Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Ngara Mei, 2025

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara amepokea kibali cha ajira kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa ajili ya utekelezaji wa ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Hivyo, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kwa nafasi zifuatazo:

1. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 4

Majukumu:

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka mbalimbali.
  • Kupokea na kuelekeza wageni.
  • Kutafuta na kuhifadhi majalada na nyaraka.
  • Kuandaa dondoo na maandalizi ya vikao.
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

Sifa za Mwombaji:

  • Elimu ya kidato cha nne au sita.
  • Stashahada (Diploma) ya Uhazili au NTA Level 6 ya Uhazili.
  • Uwezo wa hatimkato Kiswahili na Kiingereza (maneno 100 kwa dakika).
  • Ujuzi wa kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher).

Mshahara: Ngazi ya Serikali TGS C1

2. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4

Majukumu:

  • Kurekodi barua zinazoingia na kutoka.
  • Kusambaza na kurudisha majalada.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi.

Sifa za Mwombaji:

  • Elimu ya kidato cha nne au sita.
  • Cheti cha stashahada (NTA Level 6) katika fani ya utunzaji kumbukumbu.
  • Ujuzi wa kompyuta.

Mshahara: Ngazi ya Serikali TGS C1

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
  • Kuambatisha cheti cha kuzaliwa.
  • Kuwasilisha wasifu binafsi (CV) unaojitosheleza.
  • Kuambatisha vyeti vya taaluma, kidato cha nne/sita (sio “provisional” au “statement of results”).
  • Kuambatisha picha mbili (passport size) za hivi karibuni.
  • Waliosoma nje wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na NECTA/NACTE/TCU.
  • Wastaafu wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali.
  • Waajiriwa wa serikali walioko katika nafasi za kuingilia wasitume maombi.
  • Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
  • Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 12 Juni, 2025.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI:

Barua ya maombi ielekezwe kwa:

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
S.L.P 30, NGARA

Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya Ajira Portal kupitia: https://portal.ajira.go.tz

Maombi yasiyotumwa kupitia mfumo wa Ajira Portal HAYATAFANYIWA KAZI.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MTENDAJI
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
 Simu: 028 2226016 |  Barua pepe: [email protected]
Tovuti: www.ngaradc.go.tz

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.