Ajira

Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Mwanga June, 2025

Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Mwanga 02-06-2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za ajira baada ya kupokea kibali kutoka kwa Katibu Mkuu – Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kumb. Na. FA.228/613/01G/085 ya tarehe 12 Mei, 2025.

1. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 7

Majukumu ya Kazi:

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari
  • Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
  • Kutunza taarifa za safari (logbook)
  • Kufanya usafi wa gari
  • Kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa

Sifa za Mwombaji:

  • Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV)
  • Leseni ya Daraja E au C yenye uzoefu wa mwaka 1 bila kusababisha ajali
  • Cheti cha Mafunzo ya Udereva (Basic Driving Course) kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali

Ngazi ya Mshahara:

Serikali – TGS B

MASHARTI YA JUMLA:

  • Mwombaji awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 45 (isipokuwa walioko kazini serikalini)
  • Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na waeleze aina ya ulemavu kwenye mfumo
  • Ambatanisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili
  • Watumishi wa Umma waliopata sifa mpya wapitishe maombi kwa waajiri wao
  • Ambatanisha CV yenye taarifa kamili, namba za mawasiliano na wadhamini 3
  • Ambatanisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili
  • “Testimonial,” “Provisional Results,” “Statement of Results” na result slips HAZITAKUBALIWA
  • Waliomaliza masomo nje ya Tanzania wawasilishe vyeti vilivyohakikiwa na TCU, NECTA au NACTE
  • Wastaafu wa umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
  • Watumishi walioko kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba
  • Wanaowasilisha taarifa za uongo watachukuliwa hatua za kisheria
  • Mwisho wa kutuma maombi: 17 Juni, 2025

Maombi Yatumwe Kwa:

MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA MWANGA,
S.L.P. 176, MWANGA
+255 26 2757652
+255 26 2756463
[email protected]
www.mwangadc.go.tz

Njia ya Kutuma Maombi:

Wasilisha maombi kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira: https://portal.ajira.go.tz

Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu HAYATAZINGATIWA.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA MWANGA

Makala Nyingine:

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.