Ajira

Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Mji Nanyamba Mei, 2025

Mkurugenzi wa Mji Nanyamba anawatangazia Watanzania wote wenye sifa kuomba ajira kufuatia kibali cha ajira mpya kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa nafasi zifuatazo:

1. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 8

Sifa za Mwombaji:

  • Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
  • Leseni ya Daraja “E” au “C” na uzoefu usiopungua mwaka 1 bila kusababisha ajali.
  • Cheti cha Mafunzo ya Msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Majukumu:

  • Kukagua gari kabla/baada ya safari.
  • Kuwapeleka watumishi kazini.
  • Kufanya matengenezo madogo.
  • Kusambaza nyaraka, kutunza logbook na kufanya usafi wa gari.
  • Kufanya kazi zingine utakazopangiwa na msimamizi.

Mshahara:

  • Ngazi ya Mshahara: TGS B1.

2. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 9

Sifa za Mwombaji:

  • Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
  • Diploma au NTA Level 6 ya Uhazili.
  • Ufundi wa Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza (maneno 80 kwa dakika).
  • Ujuzi wa programu za kompyuta: Word, Excel, PowerPoint, Email, Internet, Publisher.

Majukumu:

  • Kuchapa nyaraka.
  • Kupokea na kuelekeza wageni.
  • Kutunza kumbukumbu, ratiba, na majalada.
  • Kuandaa vifaa vya ofisi na kusaidia vikao.

Mshahara:

  • Ngazi ya Mshahara: TGS C1.

3. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 5

Sifa za Mwombaji:

  • Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
  • Diploma (NTA level 6) katika fani ya Masjala kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.
  • Ujuzi wa Kompyuta.

Majukumu:

  • Kuorodhesha barua zinazoingia/kutoka.
  • Kusambaza na kurudisha majalada.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi.

Mshahara:

  • Ngazi ya Mshahara: TGS C1.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI:

  • Awe raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na kutaja aina ya ulemavu wao.
  • Aambatishe CV, anuani, namba ya simu, barua pepe na majina ya wadhamini 3.
  • Vyeti vya elimu na taaluma vihalalishwe na mwanasheria.
  • “Statement of Results”, “Provisional Results”, “Results Slips” havikubaliki.
  • Waombaji waliomaliza nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na NECTA, NACTE, au TCU.
  • Wastaafu wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali maalum.
  • Maombi yasiyo zingatia masharti haya hayatapokelewa.

MAELEKEZO YA UOMBANJI:

Maombi yaambatane na barua ya maombi iliyosainiwa na vyeti husika.

Barua ielekezwe kwa:

Mkurugenzi wa Mji
Halmashauri ya Mji Nanyamba
S.L.P. 1490,
NANYAMBA – MTWARA

Maombi yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira:
👉 https://portal.ajira.go.tz

Mwisho wa kutuma maombi: 09 Juni 2025

Tangazo limetolewa na:

Eng. Mshamu A. Munde
Mkurugenzi wa Mji
Halmashauri ya Mji Nanyamba

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.