Ajira

Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Madaba Mei, 2025

Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Madaba 28-05-2025, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba anatangaza nafasi za kazi kwa Watanzania wote wenye sifa stahiki, kufuatia kibali cha ajira kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Kumb. Na. FA.97/288/01/A/25 ya tarehe 25/04/2025).

Kumb. Na. MDC/CL.10/7/56 | Tarehe: 28 Mei, 2025

1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 2

Sifa za Mwombaji:

  • Kuajiriwa mwenye Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV);
  • Awe na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au NTA Level 6;
  • Uwezo wa kuchapa Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika;
  • Mafunzo ya programu za kompyuta: Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email na Publisher.

Majukumu:

  • Kuchapa nyaraka mbalimbali;
  • Kupokea na kuelekeza wageni;
  • Kutunza ratiba, kumbukumbu na miadi ya Mkuu wake;
  • Kupanga dondoo za vikao na kutunza mahitaji ya ofisi;
  • Kufanya kazi nyingine zitakazopangwa na Mkuu wa Idara.

Mshahara: TGS C1

2.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 7

Sifa za Mwombaji:

  • Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI);
  • Stashahada au NTA Level 6 ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali;
  • Ujuzi wa kompyuta.

Majukumu:

  • Kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka;
  • Kusambaza na kurudisha majalada kwa watendaji;
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi.

Mshahara: TGS C1

3.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 5

Sifa za Mwombaji:

  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV);
  • Leseni ya Daraja C au E;
  • Uzoefu wa mwaka mmoja bila kusababisha ajali;
  • Cheti cha Mafunzo ya Udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Majukumu:

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari;
  • Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi;
  • Kutunza daftari la safari, kufanya usafi wa gari na matengenezo madogomadogo;
  • Kusambaza nyaraka.

Mshahara: TGS B1

4.0 MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45;
  • Ambatanisha CV yenye maelezo ya kina, anuani ya barua, namba za simu, email, na wadhamini watatu;
  • Ambatanisha vyeti vya elimu vilivyothibitishwa na wakili: cheti cha kidato cha IV/VI, diploma, computer na kitaaluma;
  • HAKUBALIKI: Testmonial, Provisional results, Statement of results, Result slips;
  • Vyeti vya nje ya nchi vihakikiwe na TCU/NACTE/NECTA;
  • Wastaafu hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi;
  • Waliopo kazini waombe kwa kupitia waajiri wao;
  • Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria;
  • Mwisho wa kutuma maombi: 09 Juni, 2025.

5.0 JINSI YA KUTUMA MAOMBI

  • Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa ajira (Recruitment Portal):
    👉 https://portal.ajira.go.tz
  • Barua za maombi ziandikwe kwa anuani ifuatayo:

Mkurugenzi Mtendaji (W),

Halmashauri ya Wilaya ya Madaba,
38 Barabara ya Kifaguro Magingo,
S.L.P. 10, 57186 – MADABA, SONGEA.

Imetolewa na:

SAJIDU I. MOHAMED
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA

Makala Nyingine:

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.