Ajira

Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Hai June, 2025

Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Hai 02-06-2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai anatangaza nafasi za kazi kwa Watanzania wenye sifa na ujuzi, kufuatia kibali cha ajira kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 ya tarehe 29 Aprili, 2025).

1. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 11

Sifa za Mwombaji:

  • Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV)
  • Leseni ya Daraja E au C yenye uzoefu wa mwaka 1 bila kusababisha ajali
  • Mafunzo ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na serikali

Majukumu ya Kazi:

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari
  • Kuwapeleka watumishi safarini
  • Kutunza logbook na kufanya usafi wa gari
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka

Mshahara:

Ngazi ya Serikali – TGS B

2. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 5

Sifa za Mwombaji:

  • Kidato cha Nne au Sita
  • Diploma/Stashahada ya Uhazili (NTA Level 6)
  • Uwezo wa kuandika Hatimkato (maneno 100 kwa dakika, Kiswahili & Kiingereza)
  • Ujuzi wa Kompyuta: Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher

Majukumu ya Kazi:

  • Kuchapa nyaraka
  • Kupokea na kuelekeza wageni
  • Kutunza ratiba, kumbukumbu na nyaraka
  • Kuwasiliana na kusaidia Mkuu wa Idara

Mshahara:

Ngazi ya Serikali – TGS C

3. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4

Sifa za Mwombaji:

  • Kidato cha Nne/Sita
  • Diploma (NTA Level 6) ya Masijala kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali

Majukumu ya Kazi:

  • Kupanga na kuhifadhi nyaraka
  • Kutafuta kumbukumbu zinazohitajika
  • Kuweka nyaraka kwenye mafaili
  • Kushughulikia maombi ya kumbukumbu

Mshahara:

Ngazi ya Serikali – TGS C

4. MHUDUMU WA JIKONI DARAJA LA II – NAFASI 1

Sifa za Mwombaji:

  • Kidato cha Nne
  • Cheti cha mafunzo ya uhudumu wa jikoni kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali

Majukumu ya Kazi:

  • Kusafisha vyombo na maeneo ya chakula
  • Kusaidia wapishi
  • Kuweka vifaa vya mezani

Mshahara:

Ngazi ya Serikali – TGOS A

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Awe Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45
  • Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kueleza aina ya ulemavu
  • Ambatanisha CV yenye maelezo kamili, mawasiliano na wadhamini 3
  • Vyeti vya “Result Slip”, “Provisional”, “Statement of Results” havitakubaliwa
  • Vyeti vyote vya elimu na taaluma vihakikiwe na Mwanasheria/Wakili
  • Waliosoma nje ya nchi wawasilishe uthibitisho kutoka NECTA, NACTE au TCU
  • Wastaafu wa Serikali hawaruhusiwi kuomba bila kibali maalum
  • Watumishi wa Umma walioko kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba
  • Wanaowasilisha taarifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria
  • Mwisho wa kutuma maombi: 15 Juni, 2025

Barua ya maombi ielekezwe kwa:

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya Hai
3BR-TTCL-Kanisani, S.L.P. 27, Bomang’ombe – HAI, KILIMANJARO

Maombi yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia: https://portal.ajira.go.tz

Maombi nje ya utaratibu huu hayatazingatiwa.

TANGAZO LIMETOLEWA NA:

MKURUGENZI MTENDAJI –

HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI

Makala Nyingine:

  1. Nafasi Za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze June, 2025
  2. Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Manispaa Ya Shinyanga June, 2025
  3. Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Manispaa ya Shinyanga Mei, 2025
  4. Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Songea Mei, 2025

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.