Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze anatangaza nafasi za kazi kwa Watanzania wenye sifa, kufuatia kibali kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 ya tarehe 29 Aprili, 2025).
1. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI (5)
Majukumu ya Kazi:
- Kuchapa barua, nyaraka za kawaida na za siri
- Kupokea na kuelekeza wageni
- Kutunza ratiba na kumbukumbu za vikao
- Kusimamia majalada na nyaraka
- Kuandaa mahitaji ya vifaa vya ofisi
- Kazi nyingine atakayopangiwa na mkuu wake
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha Nne au Sita
- Stashahada (NTA Level 6) ya Uhazili
- Uwezo wa kuandika kwa Hatimkato maneno 100 kwa dakika moja (Kiswahili na Kiingereza)
- Ujuzi wa Kompyuta katika programu za Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, na Publisher
Mshahara:
Kwa mujibu wa viwango vya Serikali – TGS C
2. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI (4)
Majukumu ya Kazi:
- Kuwasafirisha watumishi kwa safari za kikazi
- Kusambaza nyaraka
- Kutunza log-book
- Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha Nne au Sita
- Leseni ya Daraja C au E yenye uzoefu wa mwaka 1
- Mafunzo ya msingi ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali
Mshahara:
Kwa mujibu wa viwango vya Serikali – TGS B
MASHARTI YA JUMLA:
- Mwombaji awe Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45
- Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kueleza aina ya ulemavu
- Ambatanisha CV yenye maelezo kamili, namba ya simu, barua pepe na wadhamini 3
- Vyeti vya “Result Slip,” “Provisional,” “Testimonials” havitakubaliwa
- Cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili
- Wastaafu wa Serikali hawaruhusiwi kuomba bila kibali maalum
- Watumishi wa Umma walioko katika nafasi za kuingilia wasitume maombi
- Vyeti vyote vya taaluma viwe vimehakikiwa na Mwanasheria/Wakili
- Waliosoma nje ya nchi wawasilishe uthibitisho kutoka TCU, NECTA, au NACTE
- Wanaowasilisha taarifa za uongo watachukuliwa hatua za kisheria
- Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza
- Mwisho wa kutuma maombi: 15 Juni, 2025
Maombi yote yawasilishwe kwa anuani:
MKURUGENZI MTENDAJI (W), HALMASHAURI YA WILAYA YA CHALINZE, S.L.P 65, CHALINZE.
Maombi yatumiwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira kupitia:
👉 https://portal.ajira.go.tz
Maombi nje ya utaratibu huu hayatazingatiwa.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHALINZE
Makala Nyingine: