Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Mbozi 08-06-2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa kwamba, baada ya kupata kibali cha ajira kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi wa Umma, anakaribisha maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:
1. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 5
Majukumu:
- Kuchapa barua na nyaraka za kawaida na za siri
 - Kupokea wageni na kuwapa msaada
 - Kutunza kumbukumbu za miadi na ratiba
 - Kuandaa mahitaji ya vifaa vya ofisi n.k.
 
Sifa za Mwombaji:
- Kidato cha Nne au Sita
 - Stashahada ya Uhazili (NTA Level 6)
 - Ufahamu wa Hatimkato (maneno 100 kwa dakika) kwa Kiswahili na Kiingereza
 - Ujuzi wa programu za kompyuta za ofisi
 
Mshahara: TGS C
2. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4
Majukumu:
- Kusajili barua zinazoingia na kutoka
 - Kusambaza majalada kwa watendaji
 - Kutunza na kufuatilia mzunguko wa majalada n.k.
 
Sifa za Mwombaji:
- Kidato cha Nne au Sita
 - Stashahada ya Utunzaji Kumbukumbu (NTA Level 6)
 - Ujuzi wa kompyuta
 
Mshahara: TGS C
3. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 7
Majukumu:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari
 - Kuwapeleka watumishi kazini
 - Kutunza taarifa za safari n.k.
 
Sifa za Mwombaji:
- Kidato cha Nne
 - Leseni ya Daraja E au C yenye uzoefu wa mwaka 1
 - Cheti cha mafunzo ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali
 
Mshahara: TGS B1
MASHARTI YA JUMLA:
- Mwombaji awe Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45.
 - Wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na kueleza aina ya ulemavu wao.
 - Ambatanisha:
- CV ya kina
 - Vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na wakili/mwanasheria
 - Majina ya wadhamini watatu (referees)
 - HAKUBALIKI:
 
 - Provisional results, statement of results, au slips za matokeo ya kidato cha nne/sita
 - Waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU, NECTA au NACTVET.
 - Waliostaafu bila kibali hawaruhusiwi kuomba.
 - Ajira hii si kwa waajiriwa walioko kwenye nafasi za kuingilia katika Utumishi wa Umma.
 - Maombi ya uongo yatapelekea hatua za kisheria.
 - Majina tofauti kwenye vyeti yawasilishwe na hati ya kiapo (deed poll).
 - Mwisho wa kutuma maombi: 21 Juni 2025
 
JINSI YA KUTUMA MAOMBI:
- Maombi yaambatane na barua ya maombi iliyoandikwa na kusainiwa, pamoja na vyeti husika.
 - Anwani ya barua:
 
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi
S.L.P 3
Mbozi
Tuma maombi kupitia mfumo wa kielektroniki: https://portal.ajira.go.tz/
Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu hayatafanyiwa kazi.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI
Makala Nyingine:
					






Tuachie Maoni Yako