Ajira

Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Manispaa Ya Sumbawanga Mei, 2025

Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Manispaa Ya Sumbawanga 27-05-2025, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga anatangaza nafasi za ajira kwa Watanzania wote wenye sifa stahiki kujaza nafasi kumi na moja (11) zilizotokana na kibali kutoka kwa Katibu Mkuu – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

1.0 NAFASI ZINAZOTANGAZWA

1.1 Dereva Daraja la II – Nafasi 8

Majukumu ni pamoja na:

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari;
  • Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi;
  • Kufanya matengenezo madogo ya gari;
  • Kusambaza nyaraka mbalimbali;
  • Kujaza taarifa za safari katika daftari;
  • Kufanya usafi wa gari na kazi nyingine zitakazopangiwa na mwajiri.

Sifa za mwombaji:

  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV);
  • Leseni ya daraja E au C;
  • Uzoefu wa kuendesha gari kwa mwaka mmoja bila kusababisha ajali;
  • Cheti cha mafunzo ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
    Ngazi ya mshahara: TGS B

1.2 Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 3

Majukumu ni pamoja na:

  • Kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka kwenye Rejista;
  • Kusambaza na kupokea majalada kwa watendaji;
  • Kutafuta na kurudisha nyaraka/majalada sehemu husika;
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi.

Sifa za mwombaji:

  • Cheti cha Kidato cha Nne au Sita;
  • Stashahada/Diploma (NTA Level 6) ya Utunzaji Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali;
  • Ujuzi wa kutumia kompyuta.
    Ngazi ya mshahara: TGS C

2.0 MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kutuma maombi na waeleze aina ya ulemavu waliokuwa nao kwenye mfumo.
  • Ambatanisha:
    • CV yenye maelezo ya kutosha,
    • Anuani ya barua, namba ya simu, barua pepe,
    • Majina ya wadhamini watatu wa kuaminika.
  • Ambatanisha pia vyeti halisi vilivyothibitishwa na Mwanasheria au Wakili:
    • Cheti cha kidato cha nne au sita,
    • Cheti cha taaluma (Diploma, Cheti, Degree),
    • Vyeti vya kitaaluma na kompyuta.
  • Hati za matokeo (Result slips, Provisional results, Statement of results) hazitakubaliwa.
  • Waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na kuthibitishwa na TCU, NECTA au NACTE.
  • Waliostaafu hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Wanaotuma taarifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Mwisho wa kutuma maombi: 03 Juni, 2025.

3.0 NAMNA YA KUTUMA MAOMBI

Barua ya maombi iwe imeandikwa na kusainiwa, ikiambatana na vyeti vyote muhimu. Anuani ya barua ielekezwe kwa:

Mkurugenzi wa Manispaa
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
S.L.P. 187

Maombi yote yawasilishwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal):
👉 https://portal.ajira.go.tz

Maombi yote yatakayowasilishwa nje ya utaratibu huu hayatafanyiwa kazi.

Imetolewa na:
Mangali U. E
Mkurugenzi wa Manispaa – Sumbawanga

Makala Nyingine:

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.