Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga amepokea kibali cha ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kwa nafasi zifuatazo:
1. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 04
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI).
- Diploma au NTA Level 6 katika fani ya utunzaji kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Ujuzi wa kutumia kompyuta.
Majukumu:
- Kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka kwenye rejista.
- Kusambaza na kupokea majalada kutoka kwa watendaji.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada (file tracking).
- Kupanga, kuchambua na kuhifadhi nyaraka kwa mujibu wa somo husika.
- Kuhudumia watafiti na kurudisha majalada kwenye ghala.
Ngazi ya Mshahara: TGS C1 (Ajira ya kudumu)
2. Dereva Daraja la II – Nafasi 10
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI).
- Leseni ya Daraja C au E.
- Uzoefu wa mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
- Mafunzo ya msingi ya udereva kutoka VETA, NIT au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Majukumu:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari.
- Kuwapeleka watumishi safarini.
- Kufanya matengenezo madogo, usafi na kuandika taarifa za safari kwenye daftari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka.
Ngazi ya Mshahara: TGS B1 (Ajira ya kudumu)
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45 (isipokuwa walioko Serikalini).
- CV ya kina yenye anwani, simu, na referees watatu wa kuaminika.
- Ambatanisha vyeti vya elimu (Kidato cha Nne/Sita), taaluma na cheti cha kuzaliwa.
- “Result Slip”, “Statement of Results”, “Provisional Results” HAZITAKUBALIWA.
- Waliomaliza masomo nje ya nchi wawasilishe uthibitisho kutoka NECTA au TCU.
- Maombi yawasilishwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
- Waombaji wenye ulemavu waeleze mahitaji yao kwenye barua ya maombi.
- Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
- Waliostaafu hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Mwisho wa kutuma maombi: tarehe 13 Juni, 2025.
Namna ya Kutuma Maombi:
Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa Ajira Portal: https://portal.ajira.go.tz
Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu hayatafanyiwa kazi.
Anwani ya barua:
Mkurugenzi wa Manispaa
Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa
Barabara ya Mwanza, Chamaguha
S.L.P. 28, Shinyanga
Simu: 028-2763213
Barua pepe: [email protected]
Tovuti: www.shinyangamc.go.tz
TANGAZO LA AJIRA MANISPAA YA SHINYANGA .pdf
Imetolewa na:
Mwl. Alexius R. Kagunze
MKURUGENZI WA MANISPAA – SHINYANGA