Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Manispaa Ya Bukoba 22-10-2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba amepokea kibali cha ajira chenye Kumb.Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Utawala Bora.

Anawatangazia Watanzania wote wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 2 za Msaidizi wa Kumbukumbu II kama inavyoonekana hapa chini:-

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II (NAFASI 2)

  • MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II
    1. Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye regista (Incoming correspondence register)
    2. Kuorodhesha barua    zinazotoka    nje    ya     taasisi     (Outgoing correspondence register)
  • Kusambaza majalada kwa watendaji ( Action Officers)
  1. Kupokea majalada yanayorudi masijala toka kwa watendaji
  2. Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/majalada     yanayohitajika     na watendaji
  3. Kurudisha majalada     kwenye     shubaka/kabati    la     majalada (racks/filing cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi (File Tracking)

SIFA ZA MWOMBAJI

  1. Awe amehitimu Kidato cha Nne au Sita mwenye Stashahada au NTA Level 6 katika Fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka katika Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  1. Mwombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini
  2. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.

iii.  Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma

  1. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa aajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  2. Waombaji aambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed V) yenye anawani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  3. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti ya kuzaliwa, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Testmonials” “Provisional Results”. Statement of Results”, hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  1. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu
  2. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka CCA.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  3. Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za
  • Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 04, Novemba, 2024.
  • MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

MKURUGENZI WA MANISPAA,

HALMAHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA,

S.L.P.284,

BUKOBA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira Recruitment Portal kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Seckretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment

Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Limetolewa na:

MKURUGENZI WA MANISPAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA

Nafasi Za Kazi Nyingine: