NACTVET Udahili wa Vyuo 2025/2026 (Vyuo vya Afya na Vingine) Private-binafsi na serikali, Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kufunguliwa Kwa Dirisha La Udahili Kwa Mwaka Wa Masomo 2025/2026.
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linapenda kuufahamisha umma kuwa dirisha la udahili kwa ngazi ya Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) kwa mwaka wa masomo 2025/2026 limefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 28 Mei hadi 11 Julai, 2025.
Udahili wa Vyuo 2025/2026
1.0 Namna ya Kutuma Maombi
A. Kwa Kozi Zisizo za Afya na Kozi za Afya Zanzibar:
- Maombi yatumwe mojawapo kwa moja kwenye vyuo husika kuanzia 28 Mei hadi 11 Julai, 2025.
B. Kwa Kozi za Afya Tanzania Bara:
- Maombi yatumiwe kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kupitia tovuti:
👉 www.nactvet.go.tz
2.0 Mwongozo wa Udahili
- Orodha ya vyuo na kozi zinazopatikana inapatikana kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili 2025/2026 (Admission Guidebook) kinachopatikana kupitia tovuti ya Baraza:
👉 www.nactvet.go.tz
3.0 Maelekezo kwa Wanaotuma Maombi Kupitia Mfumo wa CAS
- Muombaji anaweza kuchagua vyuo zaidi ya kimoja.
- Atapokea ujumbe wa kuthibitisha kuchaguliwa kutoka NACTVET kupitia namba ya simu aliyotumia.
- Ujumbe huo utakuwa na msimbo (code) wa kuthibitisha kwa chuo husika.
- Atasajiliwa chuoni baada ya kuwasilisha msimbo huo.
- Baada ya usajili, muombaji athibitishe usajili wake kupitia “student’s information verification” kwenye tovuti ya NACTVET.
4.0 Maelekezo kwa Wanaotuma Maombi Moja kwa Moja Vyuoni
- Muombaji anaweza kuomba chuo zaidi ya kimoja.
- Chuo kitawasilisha taarifa za muombaji kwa NACTVET kwa ajili ya uhakiki.
- Muombaji atapokea ujumbe wa kuthibitisha kuwa taarifa zake zimepokelewa na kupewa msimbo wa uhakiki.
- Baada ya kuwasilisha msimbo huo chuoni, atasajiliwa.
- Baada ya usajili, aingie www.nactvet.go.tz kuthibitisha taarifa zake kupitia “student’s information verification”.
5.0 Tahadhari Muhimu
- Mwombaji anapaswa kujaza taarifa zake kwa usahihi na umakini, na kutunza msimbo na ujumbe kutoka NACTVET.
- Epuka kumpa mtu mwingine taarifa zako ili kuepusha usumbufu wowote.
- Baraza linasisitiza ushiriki binafsi wa muombaji katika mchakato mzima wa udahili.
Imetolewa na:
Ofisi ya Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET)
Tarehe: 28 Mei, 2025
Kwa maelezo zaidi tembelea: 👉 www.nactvet.go.tz