MSAIDIZI AFYA YA MAZINGIRA II (ENVIROMENTAL HEALTH ASSISTANT II) – Nafasi 219

MSAIDIZI AFYA YA MAZINGIRA II (ENVIROMENTAL HEALTH ASSISTANT II) – Nafasi 219

MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kudhibiti na kuzuia milipuko ya magonjwa;
  2. Kupambana na kuzuia wadudu na wanyama wanaoeneza magonjwa;
  • Kusimamia uzikaji wa maiti zisizotambuliwa na zile zinazotokana na magonjwa ya kuambukiza;
  1. Kuandaa taarifa mbali mbali za Afya ya Mazingira katika ngazi ya kata na kuziwasilisha katika mamlaka husika;
  2. Kukusanya na kuchambua takwimu za Afya ya Mazingira, katika kata na kutoa mrejesho ili kuchukua hatua zinazostahili;
  3. Kutoa elimu ya afya ya mazingira kwa jamii;
  • Kukagua mazingira katika sehemu zinapotengenezwa vyakula ili kuhakikisha usalama na afya ya jamii;
  • Kusimamia sheria za afya ya mazingira katika ngazi ya Kata pamoja na kusaidia jamii katika kutengeneza sheria ndogondogo;
  1. Kuhamasisha jamii katika kuboresha vyanzo vya maji na Usafi wa Mazingira;
  2. Kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa Huduma za Afya ya Msingi katika ngazi ya Kata; na
  3. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Astashahada ya  Sayansi ya  Afya  ya  Mazingira kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA

TGHS A

MASHARTI YA JUMLA

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
  2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
  3. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa
  4. Waombaji wote  waambatishe  cheti  cha  kuzaliwa  kilichothibitishwa  na Mwanasheria/Wakili.
  1. Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba
  2. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-

Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

Computer Certificate

Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

  1. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
  2. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  3. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu
  4. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
  5. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 01 Novemba, 2025.
  6. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

KATIBU,

OFISI YA RAIS,

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,

  1. L. P. 2320,

Mtaa wa Mahakama, Tambukareli, DODOMA.

  1. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
  2. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.