Mpangilio Wa Kanda Za Usaili Wa Mahojiano Usaili Wa Mei Hadi Juni, 2025, Wasailiwa wote waliopangwa kushiriki usaili wa mahojiano kwa kipindi cha Mei hadi Juni 2025 wanasisitizwa kuzingatia mpangilio wa vituo vya usaili kama ulivyoainishwa hapa chini.
Kila msailiwa anatakiwa kufika katika Kanda ya Usaili wa Mahojiano kulingana na eneo alilofanyia usaili wa mchujo.
MPANGILIO WA KANDA ZA USAILI WA MAHOJIANO
Na. | Mahali/Mkoa wa Usaili wa Mchujo | Kanda ya Usaili wa Mahojiano | Kituo (Venue) cha Usaili wa Mahojiano |
---|---|---|---|
1 | Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga | Arusha | Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) |
2 | Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Pwani | Dar es Salaam | Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni |
3 | Dodoma, Iringa, Morogoro, Singida | Dodoma | Ofisi za Sekretariati ya Ajira Katika Utumishi wa Umma – PSRS |
4 | Mbeya, Njombe, Ruvuma, Songwe, Rukwa | Mbeya | Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) |
5 | Geita, Kagera, Simiyu, Shinyanga, Mara, Mwanza | Mwanza | Mwanza Alliance English Medium |
6 | Katavi, Kigoma, Tabora | Tabora | Shule ya Sekondari ya Wasichana – Tabora |
7 | Unguja | Unguja | Jengo la Katiba na Sheria – Mazizini |
MAELEKEZO MUHIMU:
- Wasailiwa wanaombwa kufika katika vituo vya usaili siku moja kabla ya siku ya mahojiano.
- Wajitahidi kuwa na vitambulisho halali na nyaraka zote muhimu kama zilivyoelekezwa katika barua ya kuitwa kwenye usaili.
- Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti rasmi ya Sekretariati ya Ajira: www.ajira.go.tz
MPANGILIO WA KANDA ZA USAILI WA MAHOJIANO MEI HADI JUNI 2025-1 PDF
Makala Nyingine: