Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi Jeshi la Polisi (Sample)

Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi Jeshi la Polisi (Sample), Sample ya Barua Kutuma Maombi ya ajira mpya na nafasi za kazi zilizotangazwa jeshi la polisi Tanzania PDF. 

MFANO WA BARUA YA KUOMBA KAZI JESHI LA POLISI

Jina lako
Anwani yako
Mtaa/Wilaya
Simu: XXX-XXX-XXXX
Barua pepe: BaruaYako@email.com
Tarehe: DD/MM/YYYY

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania
S.L.P 961,
DODOMA.

YAH: MAOMBI YA NAFASI YA KAZI KATIKA JESHI LA POLISI

Mheshimiwa Mkuu wa Jeshi la Polisi,

Mimi [Jina lako], raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka [XX], naomba nafasi ya ajira katika Jeshi la Polisi Tanzania kwa mwaka 2025/2026 kama ilivyotangazwa rasmi. Nina elimu ya [Shahada/Stashahada/Astashahada/Kidato cha Sita/Nne] katika fani ya [Taja fani yako].

Nina sifa zote zinazohitajika kwa mujibu wa tangazo, ikiwa ni pamoja na:

  • Afya njema na uwezo wa kimwili na kiakili.
  • Urefu wa [Taja urefu wako].
  • Uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha.
  • Sijawahi kuajiriwa katika taasisi nyingine ya serikali.
  • Niko tayari kufanya kazi mahali popote Tanzania kama itakavyohitajika.

Nimeambatanisha nakala za vyeti vyangu vya elimu, cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha taifa, na nyaraka nyingine kama uthibitisho wa sifa zangu.

Ninaomba kupatiwa nafasi hii ili kutoa mchango wangu kwa Jeshi la Polisi na taifa kwa ujumla. Natanguliza shukrani zangu kwa kuzingatia ombi langu. Natumaini nitapata fursa ya kuja kwenye usaili.

Wako mtiifu,

[Jina lako]
Saini yako

Makala Nyingine: