Matokeo ya Udahili wa Vyuo kozi za Afya 2025/ 2026 CAS awamu ya tatu

Hapa ni Matokeo ya Udahili wa Vyuo kozi za Afya 2025/ 2026 CAS awamu ya tatu CAS Selection 2025 NACTVET,

MATOKEO YA UCHAGUZI WA UDAHILI KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) KWA KOZI ZA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026 – AWAMU YA TATU

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linautaarifu umma kuwa matokeo ya uchaguzi wa awamu ya tatu kwa waombaji wa programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2025/2026 yametangazwa rasmi leo, tarehe 5 Oktoba, 2025.

Baraza liliratibu udahili wa wanafunzi kwa awamu ya tatu kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) katika kozi mbalimbali za Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2025/2026.

Jumla ya waombaji 10,622 walikamilisha maombi yao kwa kuchagua vyuo/programu walizozipenda. Kati yao, waombaji 9,697 walikuwa na sifa katika programu walizoomba, huku waombaji 925 hawakuwa na sifa stahiki.

Jumla ya waombaji 6,271 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vinavyotoa programu mbalimbali za Afya na Sayansi Shirikishi, ambapo wanawake ni 3,276 (52%) na wanaume ni 2,995 (48%). Kati yao, waombaji 194 wamechaguliwa katika vyuo vya serikali, na waombaji 6,077 katika vyuo visivyo vya serikali.

Aidha, waombaji wenye sifa ambao hawakuchaguliwa kutokana na ushindani katika programu au vyuo walivyoomba, wanashauriwa kuomba upya katika vyuo vyenye nafasi wazi kupitia dirisha la awamu ya nne na ya mwisho la udahili kupitia mfumo wa CAS.

Waombaji wote wanaweza kuangalia matokeo ya uchaguzi kupitia tovuti ya Baraza:  www.nactvet.go.tz kwa kubonyeza CAS Selection 2025 ili kupata taarifa zaidi.

Baraza linautaarifu umma kuwa dirisha la awamu ya nne na la mwisho limefunguliwa rasmi leo tarehe 5 hadi 15 Oktoba, 2025, na matokeo yake yatatangazwa tarehe 21 Oktoba, 2025.

Vilevile, kwa waombaji wanaotaka kubadilisha programu au chuo, dirisha la uhamisho litakuwa wazi kuanzia tarehe 5 hadi 15 Oktoba, 2025. Waombaji wanatakiwa kutumia akaunti zao walizotumia kuomba na kuchaguliwa kupitia tovuti ya Baraza kukamilisha maombi hayo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET)
5 Oktoba, 2025