Majina ya Walioitwa Kazini TRA 2025 PDF Download, TRA Oral Interview Results 2025: Matokeo Ya Usaili Updates, ORAL_RESULT_1.pdf Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitangaza nafasi za ajira 1,596 mnamo Februari 2025. Tangazo hilo liliibua mwitikio mkubwa kutoka kwa Watanzania, ambapo jumla ya maombi ya ajira 135,027 yaliwasilishwa.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Kati ya hao, waombaji 113,023 waliitwa kushiriki katika mtihani wa maandishi baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa. Mtihani huo wa maandishi ulifanyika tarehe 29 na 30 Machi 2025, ambapo waliopasi waliendelea katika hatua ya usaili wa ana kwa ana (oral interview).
Hatua ya Usaili wa Mdomo
Usaili wa mdomo ulifanyika kati ya tarehe 12 hadi 14 Mei 2025 na ulihusisha waombaji 6,325 waliopita mtihani wa maandishi. Hatua hii ililenga kuchuja zaidi ili kupata watu wenye sifa stahiki kuajiriwa katika Mamlaka.
Kuongezeka kwa Nafasi za Ajira
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, alitoa idhini ya kuongeza nafasi za ajira 300 zaidi. Idhini hii ilitolewa kufuatia ombi la TRA na imejumuishwa katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2025/26. Hivyo, jumla ya nafasi zilizopo sasa ni 1,896 badala ya zile 1,596 za awali.
Matokeo ya Usaili
TRA inawataarifu waombaji wote waliopata nafasi ya kushiriki katika usaili wa mdomo kuwa matokeo yatatolewa tarehe 28 Mei 2025, kupitia barua pepe walizotumia kuomba kazi.
Waombaji 1,896 walioteuliwa kuajiriwa wanatakiwa kuripoti katika vituo walivyopangiwa mnamo tarehe 2 Juni 2025, saa 1:00 asubuhi, wakiwa na nyaraka zote muhimu kama ilivyoelekezwa kwenye barua pepe zao.
Taarifa Muhimu kwa Wasiochaguliwa
Waombaji 4,429 waliopata nafasi ya usaili wa mdomo lakini hawakuchaguliwa kwa sasa, taarifa zao zitahifadhiwa kwenye mfumo wa TRA kwa ajili ya nafasi nyingine zitakazojitokeza mbeleni.
Maelezo ya Mawasiliano
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na TRA kupitia:
- Tovuti: www.tra.go.tz
- Namba za Bure (Toll Free): 0800 780078 / 0800750075 / 0800110016
- WhatsApp: 0744 23 33 33
- Barua pepe: [email protected]
“Kwa Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Imetolewa na:
Moshi Jonathan Kabengwe
Kwa niaba ya Kamishna Mkuu
Dar es Salaam, 27 Mei 2025
PDF Download, TRA Oral Interview Results
https://www.tra.go.tz/images/uploads/public_notice/english/ORAL_RESULT_1.pdf
Makala Nyingine: