Majina ya waliochaguliwa JWTZ 2025 Jeshi la Ulinzi la Wananchi, www.jwtz.go.tz 2025 News, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni taasisi ya kijeshi inayowajibika na ulinzi wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na usalama wa taifa kwa ujumla.
Kila mwaka, JWTZ hufanya mchakato wa kuandikisha vijana waliomaliza elimu ya sekondari, vyuo na wale waliopitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kujiunga rasmi na utumishi wa kijeshi.
Mwaka 2025, JWTZ kwa kushirikiana na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wametoa tangazo la majina ya vijana waliopitishwa kujiunga na Jeshi hilo baada ya kufuzu taratibu na sifa stahiki.
Sifa za Kujiunga na JWTZ
Kwa mujibu wa maelezo rasmi ya JWTZ kupitia tovuti yao, mtu anayetaka kujiunga na jeshi anapaswa kuwa na:
- Raia wa Tanzania mwenye uzalendo na maadili mema.
- Umri kati ya miaka 18 hadi 26.
- Elimu ya angalau kidato cha nne (CSE) au zaidi.
- Afya njema kimwili na kiakili (upimaji hufanyika kabla ya kupokelewa).
- Kupitia mafunzo ya JKT (Jeshi la Kujenga Taifa) ni kigezo kinachopewa kipaumbele.
- Asiwe na rekodi ya makosa ya jinai.
Majina ya Waliochaguliwa JWTZ 2025
Kwa sasa, orodha kamili ya waliochaguliwa kujiunga na JWTZ kwa mwaka 2025 bado haijatangazwa rasmi kwenye tovuti ya JWTZ (www.tpdf.mil.tz), lakini kuna uwezekano mkubwa tangazo hilo litafuata baada ya uteuzi wa vijana waliomaliza JKT kuhitimishwa.
Wanafunzi waliomaliza Kidato cha Sita mwaka 2025, tayari baadhi yao wamechaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria. Majina hayo yanapatikana kupitia:
Mwananchi Digital – Majina ya JKT 2025
Kwa kawaida, baada ya kuhitimu mafunzo ya JKT, wachache huchaguliwa kuendelea mbele na mafunzo ya kijeshi rasmi ya JWTZ.
Hatua za Kufuatilia Majina
- Tembelea tovuti rasmi ya JWTZ:
https://www.tpdf.mil.tz - Nenda kwenye sehemu ya “News” au “Announcements.”
Mara nyingi tangazo la majina huwekwa kwenye sehemu hii. - Tazama pia kurasa za mitandao ya kijamii ya JWTZ kama Facebook au Twitter kwa taarifa mpya.
- Fuatilia magazeti ya serikali kama Daily News au Habari Leo ambayo hutangaza pia majina hayo.
Wasiliana na JWTZ kwa Maelezo Zaidi
Kwa yeyote anayetaka kufahamu kuhusu utaratibu wa kujiunga, anashauriwa kuwasiliana kupitia:
- Simu: +255 737 962 064
- Barua pepe: [email protected]
Kwa vijana wenye ndoto ya kulitumikia taifa kupitia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, ni muhimu kufuatilia kwa ukaribu tangazo la majina ya waliochaguliwa 2025.
Maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja na kujiunga na JKT, kuwa na afya njema, nidhamu na elimu, huchangia kwa kiasi kikubwa nafasi ya kuchaguliwa.
Kumbuka: Tangazo rasmi litapakiwa kwenye tovuti ya www.tpdf.mil.tz, hivyo hakikisha unatembelea mara kwa mara au ujiunge na chaneli au magroup ya taarifa mtandaoni kwa ajili ya kufahamu taarifa hizi mapema.
Makala Nyingine:
- Tarehe ya kuripoti JKT 2025
- Form Six JKT Selection 2025: Waliochaguliwa JKT Kidato cha sita
- Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na JKT 2025/2026 Form Six JKT Selection
- Jinsi ya kuangalia Majina Waliochaguliwa Kidato cha Tano Form five Selection 2025
- Shule walizopangiwa form one 2025 Waliochaguliwa kidato cha kwanza
- Jinsi ya Kujiunga na JKT 2025/2026 (Mwongozo kamili)
Ndugu zangu jwtz hongeleni kwa kuzidi kulinda amani ya taifa kwa ujumla pia kwa afrika nzima ila naomba watu wenye hali za chipi pia nao mtujali kwani wengi tunamalengo ya kulitumikia jeshi letu ila inashindikana kutoka na nafasi zinapotolewa wengi hatuchaguliwi kama mm nimejalibu San ila nashindwa awamu hii naombeni mnisaidie kunichagua kwani Sina hela kila anaetaka kunisaidia aniomba hela tena nyingi wakati mm napenda jeshi tena San Kwan sasai imefika mpaka nakataa tamaa awamu hii naomba mungu anitangulie pia mnichague ahsanteni pia poleni namjukumu yakazi maafande wangu