Majina ya Wachezaji wapya wa Simba 2024/2025 Waliosajiliwa Msimu Huu

Majina ya Wachezaji wapya wa Simba 2024/2025 Waliosajiliwa Msimu Huu, tutachambua kwa kina usajili mpya wa simba dirisha la 2024/25 kwa kuangazia orodha nzima na wachezaji wapya walioitwa simba msimu mpya.

Klabu ya Simba Sports Club imejipanga kikamilifu kwa msimu wa 2024/2025 kwa kufanya usajili wa wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu ili kuimarisha kikosi chake.

Simba SC imesajili wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi, wakilenga nafasi mbalimbali uwanjani. Makala hii inaangazia wachezaji muhimu waliotambulishwa na klabu ya Simba kuelekea msimu huu mpya.

Wachezaji Waliotambulishwa Simba SC 2024/2025

Jina la Mchezaji Nafasi Kutoka Mkataba
Lameck Elius Lawi Beki Coastal Union Miaka 3
Ahoua Jean Charles Kiungo Mshambuliaji Stella Club d’Adjamé Miaka 2
Steven Mukwala Mshambuliaji Asante Kotoko Miaka 2
Joshua Mutale Kiungo Zambia Miaka 3
Abdulrazak Hamza Beki SuperSport United Miaka 2
Debora Fernandes Kiungo wa Kati Mutondo Stars Miaka 3
Augustine Okejepha Beki wa Kati Rivers United Miaka 3
Valentino Mashaka Mshambuliaji Geita Gold Miaka 2
Omary Abdallah Omary Kiungo wa Kati Mashujaa FC Miaka 2
Valentin Nouma Beki wa Kushoto FC Lupopo Mwaka 1
Karaboue Chamou Beki wa Kati Racing Club d’Abidjan Miaka 2
Yusuph Kagoma Kiungo Mkabaji Singida Fountain Gate Miaka 3
Awesu Ali Awesu Kiungo Mshambuliaji KMC Miaka 2

1. Lameck Elius Lawi

Simba SC imeimarisha safu yake ya ulinzi kwa kumsajili beki chipukizi Lameck Elius Lawi kutoka Coastal Union. Mlinzi huyu wa miaka 18 amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka mitatu, akiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Lawi ameonyesha umahiri mkubwa akiwa Coastal Union, na uwezo wake wa kucheza mipira ya juu pamoja na kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma unafanya kuwa tegemeo muhimu kwenye safu ya ulinzi ya Simba.

2. Ahoua Jean Charles

Kiungo mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Ahoua Jean Charles, mwenye umri wa miaka 22, ni moja ya usajili bora wa Simba SC msimu huu. Ahoua ametokea Stella Club d’Adjamé, akiwa mchezaji bora wa msimu wa 2023/2024 katika Ligi Kuu ya Ivory Coast. Ahoua ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao nje ya box, kutoa pasi za mwisho, na kuchezesha timu.

3. Steven Mukwala

Simba SC pia imemsajili mshambuliaji mahiri Steven Mukwala kutoka Asante Kotoko ya Ghana. Usajili wa Mukwala ni wa tatu kutambulishwa na Simba kuelekea msimu wa 2024/2025, na anatarajiwa kuleta uhai katika safu ya ushambuliaji ya Simba ambayo ilikosa makali msimu uliopita.

4. Joshua Mutale

Joshua Mutale amejiunga na Simba SC akitokea Zambia, na ni moja kati ya wachezaji walioleta matumaini makubwa kwenye safu ya kiungo. Uwezo wake wa kudhibiti eneo la kiungo ni muhimu sana kwa Simba.

5. Abdulrazack Hamza

Abdulrazak Hamza amesajiliwa na Simba SC kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini. Beki huyu mwenye uzoefu mkubwa anatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya Simba, hasa kutokana na umahiri wake wa kucheza kwenye ligi za kimataifa.

6. Debora Fernandes

Kiungo mkabaji Debora Fernandes Mavambo, mwenye uraia wa Congo Brazaville na Gabon, amejiunga na Simba SC kutoka Mutondo Stars ya Zambia. Fernandes ni mchezaji hodari wa namba 8, lakini pia ana uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji.

7. Augustine Okejepha

Simba SC imepata saini ya beki Augustine Okejepha kutoka Rivers United ya Nigeria. Okejepha ni beki wa kati mwenye uwezo mkubwa wa kukaba na kuruka mipira ya juu.

8. Valentino Mashaka

Valentino Mashaka, mshambuliaji kutoka Geita Gold, amejiunga na Simba SC baada ya kuonyesha kiwango cha juu msimu uliopita, alipofunga mabao 6 na kutoa pasi moja ya goli.

9. Omary Abdallah 

Omary Abdallah ni kiungo chipukizi aliyejiunga na Simba SC kutoka Mashujaa FC ya Kigoma. Mchezaji huyu wa miaka 23 anatarajiwa kuimarisha safu ya kiungo ya Simba kwa umahiri wake wa kuchezesha timu.

10. Valentin Nouma

Beki wa kushoto Valentin Nouma kutoka Burkina Faso amejiunga na Simba SC kwa mkataba wa mwaka mmoja, akiwa na kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi. Nouma anatarajiwa kuongeza uimara kwenye safu ya ulinzi wa kushoto ya Simba.

11. Karaboue Chamou

Karaboue Chamou, beki wa kati kutoka Ivory Coast, amejiunga na Simba SC akitokea Racing Club d’Abidjan. Uwezo wake wa kukaba na kuruka mipira ya juu unatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya Simba.

12. Yusuph Kagoma

Kiungo mkabaji Yusuph Kagoma ametambulishwa na Simba SC akitokea Singida Fountain Gate. Uwezo wake wa kudhibiti mpira na kukaba unamfanya kuwa mchezaji muhimu kwa Simba msimu huu.

13. Awesu Ali Awesu

Awesu Ali Awesu amejiunga na Simba SC akitokea KMC kwa mkataba wa miaka miwili. Kiungo huyu mshambuliaji anatarajiwa kuleta uhai na ubunifu katika safu ya ushambuliaji ya Simba.

Simba SC imefanya usajili wa maana kwa msimu wa 2024/2025, ikiwa na lengo la kuimarisha safu zote uwanjani. Wachezaji waliotambulishwa wanatarajiwa kuongeza ubora katika kikosi na kusaidia klabu kutwaa mataji ndani ya nchi na kimataifa. Usajili huu unaonyesha kuwa Simba imejipanga kikamilifu kwa changamoto za msimu mpya.

Makala Nyingine: