Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri Ya Wilaya Ya Wanging’ombe Juni, 2025
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING’OMBE 14-06-2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe anapenda kuwataarifu waombaji kazi walioomba nafasi ya Mwandazi Daraja la II kuwa usaili wa mahojiano utafanyika tarehe 27 Juni 2025. Wasailiwa walioitwa wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa:
-
Usaili utafanyika tarehe 27-06-2025 kuanzia saa 1:00 asubuhi katika ukumbi wa Wanging’ombe District Council – Hall.
-
Wasailiwa wote wanatakiwa kuvaa barakoa.
-
Waje na kitambulisho cha utambulisho (NIDA, uraia, kazi, mpiga kura, au hati ya kusafiria).
-
Waje na vyeti halisi vyote kuanzia cheti cha kuzaliwa hadi shahada kulingana na sifa ya nafasi waliyoomba.
-
Testimonials, Provisional Results, Statements of Results, na Slips za kidato cha IV na VI hazitakubaliwa.
-
Wasailiwa watajigharamia chakula, usafiri na malazi.
-
Kwa walio na vyeti vya nje ya Tanzania, wahakikishe vimeidhinishwa na NECTA, TCU au NACTE.
-
Wasioona majina yao wajue hawakukidhi vigezo – waendelee kuomba tena nafasi nyingine.
-
Kada zinazohitaji usajili waje na vyeti halisi vya usajili na leseni.
-
Wasailiwa wote wanatakiwa kuingia kwenye akaunti zao kunakili namba ya mtihani mapema.
-
Hali ya hewa ni baridi – vaa mavazi yanayostahimili baridi.
-
Kwa walio na tofauti ya majina kwenye nyaraka, waje na Deed Poll iliyosajiliwa rasmi.
Ratiba ya Usaili – Mwandazi Daraja la II
Aina ya Usaili | Tarehe | Muda | Mahali |
---|---|---|---|
Usaili wa Mahojiano | 27-06-2025 | Saa 1:00 Asubuhi | Wanging’ombe District Council – Hall |
Orodha ya Majina ya Wasailiwa Walioitwa
-
Amina Salumu Mkunza – P.O Box 778, Iringa
-
Asifiwe Kimango Mwasamya – P.O Box 02, Rungwe, Mbeya
-
Burton Abraham Kyando – P.O Box 778, Iringa
-
Christina Optuna Mwinuka – P.O Box 2324, Kilolo, Iringa
-
Faraja Daniel Mhewa – P.O Box 226, Mufindi, Iringa
-
Speransia Paskal Nyawenga – P.O Box 1613, Kinondoni, Dar es Salaam
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe
TANGAZO LA USAILI MWANDAZI.pdf KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING’OMBE 14-06-2025
Makala Nyingine:
Tags: Halmashauri