TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE 14-06-2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba ajira kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 24 hadi 28 Juni 2025. Wasailiwa walioitwa wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa:
- 
Muda na Mahali: Usaili utafanyika katika tarehe na mahali yaliyoainishwa kwa kila kada. 
- 
Barakoa (Mask): Kila msailiwa anatakiwa kuvaa barakoa. 
- 
Utambulisho: Leta mojawapo kati ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Mpiga kura, uraia, kazi au hati ya kusafiria. 
- 
Vyeti Halisi: Wasailiwa waje na vyeti halisi kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV na VI, stashahada, shahada n.k. 
- 
Hati Zisizokubalika: Statement of Results, Provisional Results, Testimonials, Form IV & VI slips hazikubaliki. 
- 
Gharama: Wasailiwa watajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi. 
- 
Uhakiki wa Vyeti vya Nje: Waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU, NECTA au NACTE. 
- 
Leseni za Kitaaluma: Kada zinazohitaji usajili, wasailiwa waje na vyeti halisi vya usajili na leseni. 
- 
Namba ya Mtihani: Nenda kwenye akaunti yako nakili namba ya mtihani mapema. Namba hazitatolewa siku ya usaili. 
- 
Hali ya Hewa: Hali ya hewa Makete ni baridi. Vaa nguo zinazofaa. 
- 
Dereva II: Walete vyeti vya mafunzo ya udereva vinavyoonyesha uhalali wa leseni daraja E au C. 
- 
Majina Tofauti: Walio na majina tofauti kwenye nyaraka, walete Deed Poll iliyosajiliwa. 
Ratiba ya Usaili – Kada ya Dereva Daraja II
| Aina ya Usaili | Tarehe | Muda | Mahali | 
|---|---|---|---|
| Usaili wa Mchujo | 24-06-2025 | Saa 1:00 asubuhi | Ukumbi wa Iwawa Sekondari | 
| Usaili wa Vitendo | 26-06-2025 | Saa 1:00 asubuhi | Uwanja wa CCM | 
| Usaili wa Mahojiano | 27-06-2025 | Saa 1:00 asubuhi | Ukumbi wa Iwawa Sekondari | 
Ratiba ya Usaili – Kada ya Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja II
| Aina ya Usaili | Tarehe | Muda | Mahali | 
|---|---|---|---|
| Usaili wa Mchujo | 27-06-2025 | Saa 1:00 asubuhi | Ukumbi wa Iwawa Sekondari | 
| Usaili wa Mahojiano | 28-06-2025 | Saa 1:00 asubuhi | Ukumbi wa Iwawa Sekondari | 
Kwa majina ya walioitwa kwenye usaili na anuani zao, tafadhali angalia kiambatanisho kamili cha tangazo (PDF).
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Makete
pdf KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING’OMBE 14-06-2025
Makala Nyingine:
 
					






Tuachie Maoni Yako