Mwongozo wa Ajira Mpya za afya 2024/2025 TAMISEMI, ajira za afya TAMISEMI 2024, Tangazo la Ajira tamisemi 2024 PDF. Tangazo limetolewa na ajira.tamisemi.go.tz wovuti Rasmi.
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wizara ya afya inaendelea na utekelezaji wa mpango wa uwekezaji katika afya ya mama na mtoto nchini Tanzania yaani Tanzania Maternal and Child Health Investment Program (TMCHIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inawatangazia wananchi wote raia wa Tanzania wenye uwezo na sifa za kujaza nafasi za ajira za 400 za Mkataba kwa Kada za Afya watakaofanya kazi katika Halmashauri mbalimbali hapa nchini.
Hivyo, wahitimu kutoka kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu na Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kuanzia tarehe 6 – 20, Desemba, 2024. Nafasi za ajira zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree).
TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA ZA MKATABA KWA KADA ZA AFYA
Wataalamu wa Kada za Afya wenye sifa wanatakiwa kufuata utaratibu ule ule wa kutuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz. Waombaji waliowahi kutuma maombi yao awali kupitia mfumo huu wanatakiwa kuhuisha taarifa zao na barua za maombi. Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-
Sifa za Kitaaluma za Waombaji wa Kada za Afya
- Daktari Daraja la II – TGHS E
Waombaji wanatakiwa kuwa na,
- Shahada ya udaktari wa binadamu kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wawe wamemaliza mafunzo ya kazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja;
- Usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika); na
- Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
Tabibu Meno Daraja la II – TGHS B
Waombaji wanatakuwa kuwa na,
- Stashahada ya Tabibu Meno (Diploma in Clinical Dentistry/NTA level 6) ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali;
- Usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika); na
- Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
Tabibu Daraja la II – TGHS B
Waombaji wanatakiwa kuwa na,
- Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali; na
- Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
Mteknolojia (Dawa) Daraja la II TGHS – B
Waombaji wanatakiwa wawe Wahitimu wa Stashahada katika fani ya Uteknolojia ya muda wa miaka mitatu katika fani ya Dawa kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wafamasia.
Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II TGHS – B
Waombaji wanatakiwa kuwa na,
- Stashahada ya Uuguzi (Diploma) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council); na
- Leseni hai kutoka Baraza la Uuuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council).
Mteknolojia Msaidizi Maabara – TGHS A
- Waombaji wawe na Astashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara ya Afya (Certificate in Health Laboratory Science) kwa muda wa miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).
- Wenye Leseni hai kutoka Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).
Mteknolojia (Mionzi) Daraja la II TGHS – B
- Wahitimu wa Stashahada katika fani ya Mionzi (Diploma in Radiology/Radiography/NTA leve 6) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na
- Wenye usajili kutoka Baraza la Wataalamu wa Mionzi Tanzania (The Medical Radiology and Imaging Professionals Council); na
- Wenye Leseni hai kutoka Baraza la Wataalamu wa Mionzi Tanzania (The Medical Radiology and Imaging Professionals Council).
Mteknolojia (Maabara) Daraja Ii
- Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara ya Afya (Diploma in Health Laboratory Sciences) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).
- Wenye Leseni hai kutoka Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).
Muuguzi Daraja La Ii
- Waombaji wawe na cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council).
- Wawe na Leseni hai kutoka Baraza la Uuuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council).
Mteknolojia Msaidizi (Dawa)
- Waombaji wawe wahitimu wa kidato cha nne wenye cheti cha miaka miwili katika fani ya teknolojia ya dawa kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza lao la Taaluma.
MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI
Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa za jumla kama ifuatavyo:
- Awe raia wa Tanzania;
- Awe na umri usiozidi miaka 45;
- Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato cha Nne, Sita, Taaluma na usajili kamili (Full Registration) au Leseni hai ya kufanya kazi ya taaluma husika);
- Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali;
- Kwa waombaji waliosajiliwa na mabaraza ya taaluma ni lazima awe na Leseni hai kutoka Baraza la taaluma yake
- Awe hajawahi kufukuzwa, kuacha kazi au kustaafishwa katika Utumishi wa Umma;
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA); na
- Aambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI WOTE
- Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi katika Halmashauri yeyote watakayopangiwa
- Waombaji wote wahakikishe wanajaza taarifa zao na kuambatisha nyaraka zote muhimu kwenye mfumo; na
- Maombi ya ajira hizi ni
WAHITIMU WALIOSOMA NJE YA NCHI
- Waombaji wote waliosoma Elimu ya Sekondari nje ya nchi wanatakiwa kupata Namba ya Ulinganifu wa Matokeo (Equivalent Number) inayoanza na Herufi EQ… kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania ili kuwawezesha kuingia kwenye Mfumo wa Ajira; na
- Waombaji waliosoma Vyuo vya Nje ya Nchi wanatakiwa kupata Ithibati ya masomo yao kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ili vyeti vyao viweze kutambuliwa na kupata uhalali wa kutumika hapa
Ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na sifa za waombaji na taratibu za utumaji wa maombi, tafadhali bofya: www.tamisemi.go.tz au wasiliana na Kituo cha huduma kwa wateja cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa namba za simu 026 2160210 au 0735 160210 kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni.
Waombaji wenye Ulemavu na sifa zilizoainishwa katika tangazo hili watume maombi yao pia kupitia mfumo. Aidha, maombi yao yaeleze aina ya ulemavu alionao na kuambatisha picha na taarifa ya uthibitisho wa Daktari kutoka katika hospitali za Serikali.
Maombi yeyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa moja Ofisi ya Rais – TAMISEMI hayatafanyiwa kazi.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 20 Desemba, 2024 saa 05:59 usiku. Tangazo hili linapatikana katika tovuti zifuatazo: www.tamisemi.go.tz
Limetolewa na:
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mji wa Serikali – Mtumba,
S.L.P 1923,
41185 DODOMA.
06 Desemba ,2024.
Leave a Reply