Tuzo za CAF 2025 CAF

Tuzo za CAF 2025 CAF Awards, Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limethibitisha kuwa washindi wa CAF Awards 2025 watatangazwa rasmi katika hafla maalumu itakayofanyika mjini Rabat, Morocco. Tukio hili limepangwa kufanyika Jumatano, Novemba 19, 2025, kuanzia saa 3:00 usiku GMT+3 (Afrika Mashariki).

Hafla ya tuzo za CAF ni miongoni mwa matukio makubwa zaidi katika kalenda ya soka barani Afrika, ikikusanya wachezaji, makocha, timu, waamuzi, na viongozi wa vyama vya soka kutoka mataifa mbalimbali.

Orodha ya Tuzo na Wagombea

Hapa chini ni wagombea waliochaguliwa katika makundi muhimu ya tuzo za CAF 2025:

Player of the Year

  • Mohamed Salah (Misri / Liverpool)
  • Achraf Hakimi (Morocco / Paris Saint-Germain)
  • Victor Osimhen (Nigeria / Galatasaray)

Goalkeeper of the Year

  • Munir Mohamedi (Morocco / RS Berkane)
  • Yassine Bonou (Morocco / Al Hilal)
  • Ronwen Williams (Afrika Kusini / Mamelodi Sundowns)

Interclub Player of the Year

  • Fiston Mayele (DR Congo / Pyramids)
  • Mohamed Chibi (Morocco / Pyramids)
  • Oussama Lamlioui (Morocco / RS Berkane)

Coach of the Year

  • Bubista (Cape Verde)
  • Mohamed Ouahbi (Morocco U-20)
  • Walid Regragui (Morocco)

Young Player of the Year

  • Abdellah Ouazane (Morocco / Ajax)
  • Othmane Maamma (Morocco / Watford)
  • Tylon Smith (Afrika Kusini / Queens Park Rangers)

National Team of the Year

  • Cape Verde
  • Morocco
  • Morocco U-20

Club of the Year

  • Pyramids
  • RS Berkane
  • Mamelodi Sundowns

Hafla ya CAF Awards 2025 si tu tukio la kusherehekea wachezaji na timu bora barani Afrika, bali pia ni fursa ya kuonyesha mafanikio ya soka wa Afrika na kuhamasisha wachezaji wachanga kuendeleza vipaji vyao.

Washindi wa tuzo hizi wanatambulika si tu kutokana na umahiri wao kwenye klabu na timu za taifa, bali pia kwa mchango wao katika maendeleo ya soka barani Afrika.

Makala Nyingine:

Droo ya makundi ya kombe la shirikisho CAF 2025/2026 Confedaration Cup

Makundi ya Klabu Bingwa Africa 2025/2026 Caf Champions League

Timu zilizofuzu Makundi Kombe La Shirikisho Africa 2025/2026 CAF

Ratiba ya Simba Robo Fainali Shirikisho CAF 2025