Matokeo na Kikosi: Yanga SC vs Bandari FC – 12 Septemba 2025

Matokeo na Kikosi: Yanga SC vs Bandari FC – 12 Septemba 2025, Ni Saa Ngapi?, Young Africans (Yanga SC) leo Ijumaa, tarehe 12 Septemba 2025, wanakipiga dhidi ya Bandari FC ya Kenya katika kilele cha Tamasha la Siku ya Mwananchi 2025.

Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utapigwa kuanzia saa 2:00 usiku, ukiwa ni sehemu ya shamrashamra za kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Young Africans Sports Club

⚽️ Official Profile Of Young Africans SC
🏆 31 Times Premier League Champions
🔰 Record – 49 Unbeaten League Games
🥈CAFCC Finalist 22/23
Makala Nyingine:

Kikosi Cha Yanga Leo Dhidi Ya Bandari

FULL 𝐓𝐈𝐌𝐄⏱️ | Young Africans SC 1-0 Bandari FC

Umuhimu wa Mchezo

Tamasha la Siku ya Mwananchi limekuwa jadi ya Yanga SC kila mwaka, ambapo mashabiki wake maarufu kama Wananchi hujitokeza kwa wingi kushuhudia kikosi kipya cha msimu.
Mchezo wa leo dhidi ya Bandari FC ni kipimo muhimu kwa benchi la ufundi la Yanga kuwapima nyota wapya waliojiunga na timu katika dirisha hili la usajili.

Miongoni mwa wachezaji wapya wanaosubiriwa kwa hamu kuonekana dimbani ni:

  • Celestin Ecua (Zoman FC)
  • Mohamed Doumbia (Majestic)
  • Balla Moussa Conte (CS Sfaxien – Tunisia)
  • Offen Chikola (Tabora United)
  • Lassine Kouma (Stade Malien)
  • Andy Boyeli (Sekhukhune – Afrika Kusini)
  • Mohammed Hussein (kutoka Simba SC)

Kikosi Cha Yanga SC Leo

Habari Web Blog itakuletea kikosi kamili cha Yanga SC kitakachoanza dhidi ya Bandari FC mara tu kitakapotangazwa rasmi na benchi la ufundi.

Bandari FC: Wageni Kutoka Kenya

Historia Fupi

Bandari FC, yenye maskani yake Mombasa, Kenya, ni moja ya timu zenye historia ndefu. Klabu hii ilianzishwa mwaka 1960 kwa jina la LASCO kabla ya kubadilika kuwa Cargo, na hatimaye kuunganishwa na Kenya Ports Authority (KPA) mwaka 1985 kuunda Bandari FC ya sasa.

Mafanikio makubwa ya Bandari ni pamoja na:

  • Mshindi wa pili wa Ligi Kuu Kenya mwaka 2017 na 2018.
  • Ubingwa wa SportPesa Super Cup 2018, uliowapa nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Licha ya kupanda na kushuka daraja mara kadhaa, Bandari imeendelea kuwa timu ya ushindani katika soka la Kenya.

Hali ya Hivi Karibuni

Msimu uliopita, Bandari ilimaliza nafasi ya 8 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Kenya kwa pointi 44.
Katika mechi tano za mwisho:

  • Sare 4 (dhidi ya Posta Rangers, Mathare United, AFC Leopards na Mara Sugar)
  • Kichapo 1 (bao 1-0 kutoka Polisi SC waliotwaa ubingwa)

Kikosi na Wachezaji Muhimu

Kikosi cha sasa cha Bandari kina wastani wa umri wa miaka 26.3, kikiwa na mchanganyiko wa wachezaji wa ndani na wa kigeni (takribani 25%).

Nyota wa kuangaliwa leo ni:

  • Joseph Okoth
  • Andrew Juma
  • Edward Satulo
  • Siraj Mohammed
  • Michael Sunday Apudo
  • Jackson Dwang (kiungo – Sudan Kusini)
  • William Wadri (mshambuliaji – Uganda, mwenye miaka 29)

Hawa ndio watakaokuwa changamoto kubwa kwa Yanga, kutokana na uzoefu wao katika ligi ya Kenya na mashindano ya kimataifa.

Kocha: Ken Odhiambo

Bandari FC kwa sasa inaongozwa na Ken Odhiambo, aliyeteuliwa Julai 2024. Ni mara yake ya tatu kurejea klabuni hapo, akichukua nafasi ya John Baraza.
Odhiambo pia ni msaidizi wa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars), Benni McCarthy.

Kurejea kwake Bandari kumeongeza matumaini ya kurejesha makali ya timu hiyo, huku akiungwa mkono na aliyekuwa kocha mkuu John Baraza kama msaidizi wake.

Mchezo wa leo kati ya Yanga SC vs Bandari FC si wa kawaida. Ni zaidi ya burudani – ni kipimo cha kikosi kipya cha Yanga na pia fursa ya Bandari kuonesha ubora wake mbele ya mashabiki wa soka la Tanzania.

Wananchi wamejiandaa kushuhudia historia ikiandikwa, na macho yote yapo pale Jangwani kuona nani ataibuka na heshima katika kilele cha Siku ya Mwananchi 2025.

FULL 𝐓𝐈𝐌𝐄⏱️ | Young Africans SC 1-0 Bandari FC