Ratiba ya Mtihani Darasa la Nne 2025 NECTA SFNA Time Table, Kwenye Makala Hii utapata Ratiba ya Mtihani Darasa la pili 2025 PDF download (SFNA timetable 2025 PDF download)
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetoa Ratiba ya Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA) kwa mwaka 2025. Kupitia makala hii, utapata ratiba kamili ya mitihani pamoja na maelekezo muhimu kwa wanafunzi na walimu. Pia tumekuwekea kiungo cha kupakua PDF ya ratiba ya SFNA 2025.
Ratiba Kamili ya SFNA 2025
Jumatano – 22 Oktoba 2025
- 2:00 – 3:30 | Sayansi (Science) – S09 / S09E
- 3:30 – 4:30 | Mapumziko
- 4:30 – 6:00 | Hisabati (Mathematics) – M08 / M08E
- 6:00 – 8:00 | Mapumziko
- 8:00 – 9:30 | Jiografia na Mazingira, Sanaa na Michezo (Geography & Environment: Arts and Sports) – A06 / A06E
Alhamisi – 23 Oktoba 2025
- 2:00 – 3:00 | Kiswahili – L01
- 3:00 – 4:00 | Mapumziko
- 4:00 – 5:00 | English Language – L02
- 5:00 – 5:30 | Mapumziko
- 5:30 – 6:30 | Lugha za Kigeni – L03 (French), L04 (Kiarabu), L05 (Kichina)
- 6:30 – 8:00 | Mapumziko
- 8:00 – 9:30 | Historia ya Tanzania na Maadili – A07
Maelekezo Muhimu kwa Wanafunzi na Walimu
- Hakikisha unayo ratiba rasmi ya mwaka 2025 iliyotolewa na NECTA.
- Soma jina la somo juu ya bahasha na uhakikishe linaendana na ratiba kabla ya kufungua.
- Kabla ya kufungua bahasha, mwanafunzi asome jina la somo kwa sauti kuthibitisha.
- Endapo kutakuwa na utofauti kati ya ratiba na karatasi ya upimaji, maelekezo ya karatasi ya upimaji ndiyo yatafuatwa.
- Wanafunzi wenye mahitaji maalum (wasioona, uoni hafifu, viziwi) waongezewe muda:
- Dakika 20 kwa kila saa kwenye somo la Hisabati.
- Dakika 10 kwa kila saa kwenye masomo mengine.
- Wanafunzi wenye uoni hafifu wapewe karatasi zenye maandishi makubwa yaliyotolewa na NECTA.
- Wanafunzi wote wanapaswa:
- Kuingia darasani nusu saa kabla ya mtihani kuanza.
- Wanaochelewa zaidi ya nusu saa hawataruhusiwa.
- Kufata maelekezo ya wasimamizi.
- Kuandika jina kamili na namba ya mtihani kwa usahihi.
- Kuepuka vitendo vya udanganyifu kwani matokeo yao yatafutwa.
Pakua Ratiba ya SFNA 2025 (PDF)
Bofya hapa kupakua Ratiba ya Mtihani wa Darasa la Nne 2025 (PDF)
https://necta.go.tz/webroot/uploads/news/SFNA_2025_EXAM_TIMETABLE.pdf
Ratiba hii ni mwongozo muhimu kwa wanafunzi wa Darasa la Nne wanaotarajia kufanya Mtihani wa Kitaifa (SFNA) mwaka 2025. Wazazi, walimu na wanafunzi wanashauriwa kuisoma kwa makini na kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
Makala Nyingine:
- Matokeo ya darasa la Nne 2024/2025 SFNA results
- NECTA Yatangaza Matokeo ya kidato cha nne 2024/2025 (Form Four Results CSEE)
- Vyuo vya ualimu ngazi ya cheti
- Shule za Advance na Combination zake 2025 Kidato cha Tano na Sita
- Combination Form Five TAMISEMI Selform jisajili online
Tuachie Maoni Yako