Ratiba ya Robo Fainali ya CHAN 2025 (Team zilizofuzu)

Ratiba ya Robo Fainali ya CHAN 2025 (Team zilizofuzu), Mashindano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani ya Nchi (CHAN 2025) yanaendelea kutimua vumbi barani Afrika, ambapo sasa yametinga katika hatua ya robo fainali. Hatua hii inakusanya timu bora zilizopambana vikali katika makundi yao, zikionesha ubora wa kandanda la ndani na kuwapa mashabiki burudani ya aina yake.

Katika hatua ya makundi, tumeshuhudia ushindani mkali, matokeo ya kushtua na ubora wa wachezaji wanaowakilisha ligi za ndani. Sasa macho yote yanahamia katika robo fainali ambapo hakuna nafasi ya makosa, kwani kila timu inapambana kuhakikisha inatinga nusu fainali na hatimaye kuwania taji hilo la kifahari.

Timu Zilizofuzu Robo Fainali ya CHAN 2025

Baada ya michezo ya makundi kukamilika, timu zilizofanikiwa kutinga robo fainali ni:

Kenya – wenyeji wa michuano, waliopata nafasi baada ya kuongoza kundi lao kwa ushindi muhimu dhidi ya wapinzani wakubwa.

Madagascar – timu iliyoonyesha kandanda safi na ubunifu mkubwa, ikiweka historia kwa kufika hatua hii.

Tanzania – Taifa Stars wakiwa na faida ya kucheza nyumbani katika michezo ya Dar es Salaam, wana matumaini makubwa ya kutinga nusu fainali.

Morocco – mabingwa wa zamani wa CHAN, wanaokuja na uzoefu na wachezaji wenye ubora wa hali ya juu.

Timu zingine mbili kutoka makundi tofauti ambazo zitasubiriwa kujulikana rasmi katika mechi zilizopangwa kufanyika visiwani Zanzibar na nchini Uganda.

Ratiba ya Robo Fainali ya CHAN 2025

Mashabiki wanatarajia burudani kubwa kutoka katika mechi hizi:

Ijumaa, 22 Agosti 2025

  • ⏰ 17:00 – Kenya v MadagascarMoi Sports Centre Kasarani, Nairobi
  • ⏰ 20:00 – Tanzania v MoroccoBenjamin Mkapa Stadium, Dar es Salaam

Jumamosi, 23 Agosti 2025

  • ⏰ 17:00 – Robo Fainali 3Amaan Stadium, Zanzibar
  • ⏰ 20:00 – Robo Fainali 4Mandela National Stadium, Uganda

Ratiba ya Nusu Fainali

Baada ya robo fainali kukamilika, timu nne zitakazoshinda zitakutana tena hatua ya nusu fainali:

Jumatano, 26 Agosti 2025

  • ⏰ 17:30 – Nusu Fainali 1Benjamin Mkapa Stadium
  • ⏰ 20:30 – Nusu Fainali 2Mandela National Stadium

Ratiba ya Mchezo wa Kufutia Nafasi ya Tatu na Fainali

Ijumaa, 29 Agosti 2025

  • ⏰ 18:00 – Mchezo wa Kusaka Nafasi ya TatuMandela National Stadium

Jumamosi, 30 Agosti 2025

  • ⏰ 18:00 – Fainali KuuMoi Sports Centre Kasarani, Nairobi

Robo fainali ya CHAN 2025 inatarajiwa kuwa na mvuto wa kipekee, hasa kwa nchi za Afrika Mashariki ambazo kwa mara ya kwanza zimepata nafasi kubwa ya kuonyesha uwezo wao. Kenya na Tanzania zinapewa nafasi kubwa kutokana na faida ya nyumbani, lakini timu kama Morocco na Madagascar zinaweza kutoa upinzani mkali.

Mashabiki barani Afrika na duniani kwa ujumla wanatarajia kuona burudani ya kiwango cha juu, huku kila mechi ikiamua hatma ya timu kuelekea nusu fainali na hatimaye fainali ya kifahari jijini Nairobi.

Makala Nyingine;