Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri Ya Wilaya Ya Makete Juni, 2025
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE 14-06-2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba ajira kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 24 hadi 28 Juni 2025. Wasailiwa walioitwa wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa:
-
Muda na Mahali: Usaili utafanyika katika tarehe na mahali yaliyoainishwa kwa kila kada.
-
Barakoa (Mask): Kila msailiwa anatakiwa kuvaa barakoa.
-
Utambulisho: Leta mojawapo kati ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Mpiga kura, uraia, kazi au hati ya kusafiria.
-
Vyeti Halisi: Wasailiwa waje na vyeti halisi kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV na VI, stashahada, shahada n.k.
-
Hati Zisizokubalika: Statement of Results, Provisional Results, Testimonials, Form IV & VI slips hazikubaliki.
-
Gharama: Wasailiwa watajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
-
Uhakiki wa Vyeti vya Nje: Waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU, NECTA au NACTE.
-
Leseni za Kitaaluma: Kada zinazohitaji usajili, wasailiwa waje na vyeti halisi vya usajili na leseni.
-
Namba ya Mtihani: Nenda kwenye akaunti yako nakili namba ya mtihani mapema. Namba hazitatolewa siku ya usaili.
-
Hali ya Hewa: Hali ya hewa Makete ni baridi. Vaa nguo zinazofaa.
-
Dereva II: Walete vyeti vya mafunzo ya udereva vinavyoonyesha uhalali wa leseni daraja E au C.
-
Majina Tofauti: Walio na majina tofauti kwenye nyaraka, walete Deed Poll iliyosajiliwa.
Ratiba ya Usaili – Kada ya Dereva Daraja II
Aina ya Usaili | Tarehe | Muda | Mahali |
---|---|---|---|
Usaili wa Mchujo | 24-06-2025 | Saa 1:00 asubuhi | Ukumbi wa Iwawa Sekondari |
Usaili wa Vitendo | 26-06-2025 | Saa 1:00 asubuhi | Uwanja wa CCM |
Usaili wa Mahojiano | 27-06-2025 | Saa 1:00 asubuhi | Ukumbi wa Iwawa Sekondari |
Ratiba ya Usaili – Kada ya Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja II
Aina ya Usaili | Tarehe | Muda | Mahali |
---|---|---|---|
Usaili wa Mchujo | 27-06-2025 | Saa 1:00 asubuhi | Ukumbi wa Iwawa Sekondari |
Usaili wa Mahojiano | 28-06-2025 | Saa 1:00 asubuhi | Ukumbi wa Iwawa Sekondari |
Kwa majina ya walioitwa kwenye usaili na anuani zao, tafadhali angalia kiambatanisho kamili cha tangazo (PDF).
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Makete
pdf KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING’OMBE 14-06-2025
Makala Nyingine:
Tags: Halmashauri