Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Biharamulo Mei, 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo amepokea kibali cha utekelezaji wa ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kwa nafasi zifuatazo:

1. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 05

Majukumu ya Kazi:

  • Kuchapa barua na nyaraka za kawaida na siri.
  • Kupokea na kusaidia wageni.
  • Kutunza ratiba na kumbukumbu za mkuu wake.
  • Kuandaa vikao na mahitaji ya ofisi.

Sifa za Mwombaji:

  • Elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
  • Diploma au NTA Level 6 ya Uhazili.
  • Uwezo wa hati mkato maneno 100 kwa dakika kwa Kiswahili na Kiingereza.
  • Ujuzi wa programu za kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Email, Publisher).

Ngazi ya Mshahara: TGS C

2. Dereva Daraja la II – Nafasi 06

Majukumu ya Kazi:

  • Kukagua gari kabla/baada ya safari.
  • Kuwapeleka watumishi safarini.
  • Kufanya usafi na matengenezo madogo ya gari.
  • Kutunza kumbukumbu za safari.

Sifa za Mwombaji:

  • Elimu ya kidato cha Nne.
  • Leseni ya Daraja C au E.
  • Uzoefu wa mwaka 1 bila ajali.
  • Mafunzo ya msingi ya udereva kutoka VETA, NIT au chuo kinachotambulika.

Ngazi ya Mshahara: TGS B

3. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 04

Majukumu ya Kazi:

  • Kutafuta, kupanga na kuhifadhi kumbukumbu.
  • Kuweka nyaraka kwenye majalada na reki.
  • Kuhudumia maombi ya kumbukumbu kutoka taasisi mbalimbali.

Sifa za Mwombaji:

  • Elimu ya kidato cha Nne au Sita.
  • Diploma (NTA Level 6) ya Utunzaji wa Kumbukumbu katika fani za Afya, Masjala, Mahakama au Ardhi.

Ngazi ya Mshahara: TGS C

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Awe raia wa Tanzania, umri miaka 18–45 (isipokuwa walioko serikalini).
  • Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja aina ya ulemavu kwenye mfumo.
  • Ambatanisha cheti cha kuzaliwa na nakala ya kitambulisho cha NIDA.
  • Ambatanisha CV, vyeti vya taaluma, kidato cha nne/sita na mafunzo ya kazi.
  • Ambatanisha picha moja ya passport size (iandikwe jina nyuma).
  • “Statement of Results” hazitakubaliwa.
  • Waliosoma nje wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU/NACTE/NECTA.
  • Waajiriwa wa Serikali walioko kwenye nafasi za kuingilia wasitume maombi.
  • Maelezo ya kughushi yatapelekea hatua za kisheria.
  • Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 06 Juni, 2025.

MUHIMU:

Barua ya maombi iliyosainiwa ielekezwe kwa:

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 70,
BIHARAMULO

Namna ya Kutuma Maombi:

Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa Ajira (Recruitment Portal) kwa kutumia kiunganishi: https://portal.ajira.go.tz

Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu hayatazingatiwa.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MTENDAJI WA WILAYA
HALMASHAURI YA WILAYA YA BIHARAMULO