Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Bumbuli
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli amepokea kibali cha ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo, anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kwa nafasi zifuatazo:
Contents
hide
1. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 03
Sifa za Mwombaji:
- Awe amefaulu Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
- Awe na Stashahada (Diploma) au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili.
- Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa maneno 100 kwa dakika.
- Awe na ujuzi wa kutumia programu za ofisi kama Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail, na Publisher.
Majukumu:
- Kuchapa barua na nyaraka za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni na kuelekeza wapi pa kupata huduma.
- Kutunza kumbukumbu na ratiba za kazi za mkuu wake.
- Kutafuta na kuratibu majalada/nyaraka.
- Kuandaa dondoo na vifaa vya mikutano.
Mshahara:
Ngazi ya mshahara wa Serikali – TGS C.
2. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 05
Sifa za Mwombaji:
- Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV).
- Awe na leseni ya daraja ‘C’.
- Uzoefu wa kuendesha gari angalau mwaka 1 bila kusababisha ajali.
- Awe amehitimu mafunzo ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Majukumu:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari.
- Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo ya gari.
- Kutunza daftari la safari (log book).
- Kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kusafisha gari na kazi nyingine kama atakavyoelekezwa.
Mshahara:
Ngazi ya mshahara wa Serikali – TGS B.
3. MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Awe Mtanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
- Awe na cheti cha kuzaliwa.
- Awasilishe wasifu binafsi (CV) yenye anuani, namba za simu na majina ya wadhamini.
- Ambatanisha nakala za vyeti vya kitaaluma, kidato cha Nne/Sita na mafunzo mengine.
- “Statement of Results” au “Provisional Results” hazitakubalika.
- Ambatanisha picha mbili (passport size) za hivi karibuni.
- Waliosoma nje wahakikishe vyeti vyao vimeidhinishwa na TCU/NECTA/NACTE.
- Wastaafu wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali maalum.
- Waombaji walioko katika utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba kwa nafasi hizi za kuingilia.
- Wanaotoa taarifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi: 09 Juni 2025
4. MAELEKEZO YA KUTUMA MAOMBI:
Barua ya maombi iliyosainiwa iambatishwe na vyeti muhimu na iandikwe kwenda kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli, S.L.P. 111,
BUMBULI.
Njia ya kutuma maombi:
Wasilisha maombi kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal): https://portal.ajira.go.tz
Imetolewa na:
Baraka M. Zikatimu
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli