Ajira

Nafasi Za Kazi Ofisi Ya Waziri Mkuu-sera,bunge Na Uratibu Mei, 2025

Tangazo La Nafasi Za Kazi Ofisi Ya Waziri Mkuu-sera,bunge Na Uratibu 23-05-2025,  Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi nane (08) kama ifuatavyo:

1. MPIGA CHAPA MSAIDIZI DARAJA II (ASSISTANT PRINTER II)

Idadi ya Nafasi: 08
Mahali: Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu

1.1 Majukumu ya Kazi

  • Kukunja karatasi ngumu na kutengeneza jalada (covers) za vitabu, majarida na madaftari kwa njia ya kugandisha, kushona au kuunganisha.
  • Kukarabati vitabu au kumbukumbu kwa kuweka jalada jipya au kurudisha katika hali ya awali.
  • Kupanga vifaa vilivyotengenezwa kwa vipimo au seti husika.
  • Kuendesha mashine za kupiga chapa, kukata karatasi, kushona au kugandisha vitabu kwa mujibu wa ubora unaotakiwa.
  • Kupanga karatasi za kuchapwa kwa hesabu ya kila nakala (kitabu, jarida, daftari, n.k).

1.2 Sifa za Muombaji

  • Awe amehitimu kidato cha Nne au Sita katika masomo ya Sayansi au Sanaa.
  • Awe na cheti cha Trade Test daraja la I au Level III katika Lithography, Composing, Binding au Machine Binding.
  • Au awe amehitimu mafunzo ya miaka miwili ya kupiga chapa.

1.3 Ngazi ya Mshahara

  • Kwa mujibu wa viwango vya Serikali: TGS B

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  1. Awe Raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45 (isipokuwa kwa walioko kazini Serikalini).
  2. Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja aina ya ulemavu kwenye mfumo wa maombi.
  3. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na mwanasheria/wakili.
  4. Watumishi wa Umma wanaotaka kuhamia kada nyingine lazima wapitishe barua zao kwa waajiri wao wa sasa.
  5. Maombi yaambatane na:
    • CV iliyoandikwa kwa kina (anwani, simu, na majina ya wadhamini watatu).
    • Nakali halisi zilizothibitishwa za vyeti vya taaluma na kitaaluma:
      • Cheti cha kuzaliwa
      • Cheti cha kidato cha Nne na Sita (kwa waliofikia)
      • Vyeti vya mafunzo ya ufundi/stashahada/astashahada
      • Vyeti vya kompyuta
      • Vyeti vya kitaaluma (kutoka bodi husika)
    • HAKUTAKUBALIWA: “Provisional Results”, “Statement of Results”, na “Slips”.
  • Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuthibitishwa na NECTA, NACTE au TCU.
  • Waliostaafu Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa idhini ya Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji walioajiriwa katika nafasi sawa za kuingilia katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.
  • Watakaotoa taarifa au vyeti vya kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.

MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 05 Juni, 2025

MAELEKEZO YA UWASILISHAJI WA MAOMBI:

Maombi yote ya kazi yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia Mfumo wa Ajira wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma https://portal.ajira.go.tz/user/auth/login. Kumbuka kuambatisha barua ya maombi iliyoandikwa kwa ufasaha, imesainiwa na kuelekezwa kwa:

KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Makala Nyingine:

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.