TANGAZO LA KUITWA KAZINI Tarehe: 24 Aprili 2025 Taasisi Mbalimbali za Umma
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa waombaji kazi waliopitia usaili kati ya tarehe 10 Septemba 2024 hadi 24 Februari 2025, matokeo yao rasmi yamekamilika. Waombaji waliofaulu wamepangiwa vituo vya kazi katika taasisi mbalimbali za umma na orodha kamili ya majina yao imeambatanishwa katika tangazo hili.
Orodha hii pia inajumuisha waombaji waliokuwa katika kanzidata kwa kada mbalimbali, ambao wamepata nafasi rasmi za kazi baada ya nafasi hizo kupatikana.
MAELEKEZO KWA WALIOFAULU
1. Kupata Barua za Kazi
Waliofaulu na kupangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kufungua akaunti zao kupitia mfumo wa Ajira Portal, sehemu ya “My Applications”. Barua za kupangiwa vituo vya kazi zinapatikana hapo, na wanapaswa kupakua (download) na kuchapisha (print) barua hizo kwa ajili ya kuziwasilisha kazini.
2. Kuripoti kwa Mwajiri
Kabla ya kupewa barua ya ajira, wahusika wanapaswa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa ndani ya muda uliowekwa katika barua husika, wakiwa na nyaraka zifuatazo:
- Vyeti halisi vya taaluma kuanzia kidato cha nne na kuendelea
- Kitambulisho halali (kama NIDA, leseni ya udereva, au pasipoti)
- Barua iliyopakuliwa kutoka Ajira Portal
Mwajiri atafanya uhakiki wa nyaraka kabla ya utoaji wa barua rasmi ya ajira.
3. Kwa Waliokosa Nafasi
Waombaji ambao majina yao hayapo kwenye tangazo hili wanatakiwa kufahamu kuwa hawakupata nafasi kwa wakati huu. Wanaombwa kuendelea kufuatilia matangazo mengine na kuomba nafasi nyingine pindi zitakapotangazwa rasmi.
TAARIFA ZA ZIADA
Tovuti rasmi kwa ajili ya kupata barua na maelezo zaidi ni:
https://portal.ajira.go.tz
Imetolewa na:
Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Tarehe: 24 Aprili 2025
PDF Nzima Hapa; TANGAZO LA KUITWA KAZINI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA 24-04-2025
Tags: KUITWA KAZINI