Mchungaji wa Kanisa la Fellowship Baptist Church lililopo Johannesburg Nchini Afrika Kusini ambaye alitekwa na Watu wenye silaha wakati akihubiri Kanisani April12, 2025, amepatikana akiwa hai baada ya Polisi kujibizana kwa risasi na Watu waliokuwa wakimshikilia baada ya kumteka.
Taarifa kutoka Johannesburg zimeeleza kuwa bado haijawekwa wazi nia ya Watekaji hao ilikuwa ni nini lakini majibizano hayo ya risasi kati ya Polisi na Watekaji, Watu watatu wamepoteza maisha.
Mchungaji huyo aitwae Josh Sullivan (45) ambaye ni Raia wa Marekani, alitekwa wakati akihubiri mbele ya Waumini wake ambapo Watekaji hao walipora simu za Waumini na kisha kuondoka na Mchungaji huyo.
Johannesburg ni miongoni mwa Majiji 20 yanayotajwa kuwa hatari zaidi duniani kutokana na vitendo vya kihalifu, usalama mdogo pamoja na matukio ya utekaji ambayo yamekuwa yakiripotiwa kwa wingi.
Makala Nyingine:
Leave a Reply